The House of Favourite Newspapers

Chombezo: Utamu Usioisha Hamu -01

0


Ndani ya gari aina ya Jeep nyeusi alikuwa akisikiliza muziki laini kabisa! Mawazo yake mengi ni kuhusu mkutano wake atakaofanya na wafanyabiashara kutoka China.
Mzee Mombasa alihitaji kupanua wigo wa biashara zake na kuzifanya za kimataifa zaidi, hakutaka kuwa mfanyabiashara wa ndani pekee, alihitaji mataifa makubwa kumtambua na kukuza uchumi wa Tanzania.
Safari yake ingeishia Hoteli ya Holiday Inn. Pamoja na kuwa ni mfanyabiashara mkubwa nchini, alikuwa na sifa kubwa ya ubahili. Na hiki ndicho kilichomfanya akawa tajiri, maana kutoa pesa bila sababu zake za msingi, ilikuwa ngumu. Katika ujana wake hakuwahi kuwa na mwanamke mwingine mpaka alipomuoa Sabrina ambaye kwasasa anaitwa mama Defrine.
Mwanaume huyu ni tajiri mkubwa, ana biashara nje na ndani ya nchi na siku hiyo alikuwa akienda kwenye kikao cha biashara ambako ndani ya mkoba wake (breafcase) kulikuwa na mamilioni ya dola za Kimarekani.
Kila mara saa yake aliitizama kuona kama amechelewa mkutano na wafanyabiashara wenzake.
Sasa alikaribia lango la kuingia hoteli hiyo. Ghafla kuna kitu alikiona na kushtuka sana. Alihiyari kupunguza mwendo na hatimaye kufunga breki kabisa. Macho yake yalikumbana na msichana mzuri sana. Hakuwa na tabia za kutamani wanawake hovyo, ajabu kwa siku hii mwanaume aliduwaa kitambo asijue afanye nini kuweza kuthibiti hali hii mpya iliyoingia katika mfumo wake wa akili.
“Mombasa, jifanye kama hujaona kitu, hebu acha tamaa…” alifunika macho yake kwa kiganja kusudi asimuone yule binti, ajabu ni kwamba macho yalizidi kuchungulia, akaachia uso wake sehemu za macho na kushuka zipu ya suruali yake, akamgusa mwanaume mwenzake.
“Sikiliza, nilishakuonya kupenda hovyo, kwanini lakini…sasa huyo mwanamke unayechanganyikiwa naye ana kitu gani kipya kinachomshinda mkeo? Hebu acha tamaa…” Mombasa alijiambia ndani ya nafsi yake, ingawa ilionekana nafsi yake imegoma kabisa kumsikiliza. Aliendelea kuduwaa.
Msichana aliyekatisha mbele yake aliumbika kila idara, sio mguu, sura, figa namba nane, wowowowooo! Macho makubwa kiasi ya kulegea, rangi bomba nakadhalika. Zaidi alikuwa akitembea kikike na maringo kama vile mrembo wa dunia.
Mzee Mombasa tangu kumuona mrembo huyo moyo wake ukaingia na udhaifu fulani ambao mwenyewe hakuuelewa. Udhaifu wa kupenda ghafla.
“Mmh! Ni mzuri sana, sijui anakula nini, wasichana wa siku hizi wanavutia sana ila huyu amezidi, nimempenda na ameniteka hisia zangu zote!” Alijisemea moyoni akimkodolea macho udenda ukimtoka, akashusha kioo cha gari lake taratibu na kumuita jina la kutunga(jina bandia).
“Hey! Baby!” Alitokwa na kauli hiyo, hata hivyo msichana huyo hakugeuka na badala yake alikuwa sasa amempa mgongo, hali iliyozidi kumchosha akili Mombasa.
Habari za mkutano alizisahau wakati huu, akili yake ikatekwa na kimwana wa kiafrika, uzalendo ukamshinda akashuka garini akimfuata kwa nyuma bila kujali ni mke wa mtu au angeweza kupewa majibu mabaya na pengine kumharibia siku yake.
“Samahani, binti!” Wakati huu alimkaribia na kutokwa na sauti nzito ya kukwaruza.
Msichana akageuka na kukutana na sura ya mwanaume wa makamu, kwa kumwangalia alielewa mtu aliyesimama mbele yake haikosi umri wake ulikuwa ni miaka kati ya 45 au 50.
“Sema shida yako, nina haraka kidogo!” Alionekana msichana mwenye uwezo, mkufu wake wa dhahabu ulizidi kumpendezesha, tena kuna jina lililosemeka katika mkufu huo, Monica Gama. Kabla hajaendelea kuongea au kujibiwa na Mzee Mombasa, mara simu ya msichana mwenye mkufu wa Monica Gama ikaanza kuita.
“Sorry!” Kabla ya kupokea simu sauti hii ikamtoka mrembo na kupokea simu.
“Haloo! Daddy..I’m Coming…,” alisema kwa sauti ndogo iliyopoa.
Akatulia nukta kadhaa nakuendelea…”Dakika tano, nitakuwa nimefika…” Alimjibu na kukata simu. Mzee Mombasa akajua kwa huenda msichana huyo kweli alikuwa anawahi mahala.
“Okay, najua una haraka ila.. mmh! Yah! Naitwa Momba Gems, ni mfanya biashara wa kimataifa… nipo Tanzania kwa takribani mwezi mmoja hivyo ningependa uwe mwenyeji wangu, unipe kampani…,”alisema kwa kujikaza, hakujua jibu gani lingemwangukia.
“Mmh! Kampani gani, unanifahamu mimi?” Yule msichana mzuri kwa akila kitu alimuuliza.
“Sikufahamu, ndiyo mwanzo wa kujuana huko! Na kampani yangu ni kustarehe na kunionesha kila ukanda wa Tanzania!”
“Okay, kwa kifupi mi’mke wa mtu, siruhusiwi na mume wangu kuongozana na wanaume nisiowafahamu na hata ninaowafahamu…mume wangu ana wivu sana…unaona pete hii…nitawezaje kutoka na wewe?” Alisema kwa sauti ya kawaida iliyopoa, Mombasa akashusha pumzi ndefu na kumwangalia mrembo aliyekuwa mbele yake, akatizama kidole chenye pete, akamwonyesha naye pete ya ndoa, tena ya gharama kubwa.
“Nashukuru kuniambia ukweli kwamba umeolewa, mimi pia nimeoa na naipenda sana ndoa yangu, na siri ambayo naweza kukuambia sijawahi kuwa na msichana mwingine tangu nimezaliwa, ila mke wangu Mama Defrine…Ok, nisikupotezee muda, naomba uchukue Business card yangu utanipigia…,” Msichana huyo akanyoosha mkono kuchukua kadi.
“Samahani, pia kuna zawadi yako nataka kukupatia, njoo uichukue..” msichana aliridhia na kutembea kimadaha hadi lilipokuwa Jeep la Mombasa akasimama nje na sekunde kadhaa Mombasa alivuta mkoba wake wenye pesa na kuufungua.
Hapakuwa na pesa za Kitanzania au Kenya, zote zilikuwa dola za Kimarekani.
“Chukua hizi zitakusaidia kama nauli!” Alisema Mombasa, msichana huyo hakuamini, aliona kama mzaha. Akazihesabu zilikuwa , dola mia nane!
“Loh! Ahsante sana!” Monica alisema na kutabasamu na kumkumbatia Mombasa kwa furaha.
“Chukua namba zangu hizi, ila usinipigie nitakupigia wala kuandika meseji, mume wangu ana wivu na hupekenyua simu yangu anapoitilia mashaka!” Monica alisema kusoma namba za simu kwenye Business Card na kumbip Mzee Mombasa, akazisevu.
“Utanipigia saa ngapi?” Alihoji Mzee Mombasa aliuliza akimwangalia kimatamanio. Chezea kupenda weweee!!!.
“Saa tisa jioni, usizime simu!” Monica alisema na kumuaga Mombasa.
Mzee Mombasa alijishangaa sana, maishani mwake hakuwahi kupenda haraka kiasi hicho, aligundua kumbe hakuwahi kukutana na mwanamke anayempenda, sasa alishampata na alikuwa tayari kumpatia kila kitu anachokitaka juu ya mgongo wa dunia.
Hata alipokuwa ndani ya kikao, mawazo mengi yalikuwa juu ya mrembo aliyekutana naye muda mfupi. Alisahau mambo mengi aliyopanga kuzungumzia, hivyo alikumbushwa na meneja wake.
Hata meneja alihisi huenda mzee ana matatizo ya kifahamilia, ndiyo maana alionekana mwenye msongo wa mawazo na wakati mwingine atikise kichwa.
Baada ya kikao kuisha Mzee Mombasa aliangalia tena saa yake na kugundua ilikuwa saa 8. 45 mchana, hamu ya kuongea na Monica akamjia, sura yake ikamjia na kujikuta msumari wake ukipatwa na msisimko wa ajabu, dakika kumi na tano akaziona kama mwaka, kuna wakati alitamani kumpigia simu akaona ni hatari, yule ni mke wa mtu na huenda yupo na mumewe na asingependa lawama za kuvunja ndoa hiyo.
**
Monica alipofika nyumbani, kitu cha kwanza ni kuzihakiki pesa hizo kama ni halali, ni kweli zilikuwa fresh! Mumewe hakuwepo, alikuwa kibaruani ambako anafanya kazi ya kusuka wanawake nywele na hata kuwatengeneza mitindo ya kila aina. Saluni yao ilikuwa maeneo ya Mwenge, wakati wao wanaishi Ubungo maziwa.
“Hivi yule mwanaume ana pesa ngapi, yaani ananipatia utajiri, hapo ni kusalimiana, je nikimpa chakula changu cha usiku itakuwaje?”
Monica aliwaza sana, moyoni akajiambia lazima afanye mbinu za kuchukua pesa hizo za Mombasa na kufungua biashara zake, hakutaka tena kuwa mama wa nyumbani na kusubiri kuletewa na mumewe.
Alijikuta akichukua kadi ya simu na kumpigia mzee Mombasa.
“Shikamoo Momba….”
“Marahabaa hujambo mwanamke mzuri kama pesa…”
“Sijambo, vipi unaendeleaje?”
“Nipo salama, nilikuwa natamani kukupigia ila nimeogopa nikohofia huenda upo na mumeo…”
“Hapana, mume wangu hurudi usiku sana, kazi zake hazimruhusu kurudi mapema nyumbani…”
“Okay, jambo jema tunaweza kuonana tafadhali…”
“Nipo nyumbani tayari…”
“Wapi?”
“Ubungo…” Monica hakutaka kumwambia ni Ubungo Maziwa.
“Basi, chukua teksi nitalipa uje Posta…tafadhali…”
“Mmh! Mbona mbali sana, sogea karibu na ubungo…ukikaribia niambie nitatoka…sitaki kwenda mbali sana, mume wangu akirudi na kunikosa nyumbani, nitanifokea…”
“Unadhani nije wapi?”
“Sijui, angalie mwenyewe Sinza…”
“Sawa, nakuja….nakupenda sana mwanamke wa maisha yangu…” Mzee Mombasa alijikuta akitokwa na kauli hiyo.
**
Monica alishaingiwa na tamaa, alichokifanya ni kuingia bafuni kuoga. Alimuogesha mwenye jina kwa makini sana, huyu akimwambia “Uwe mwaminifu katika ndoa yako, habari za kudanga sitaki, yule nitamchuna tu pesa zake,” ndivyo alivyojiaminisha na kujihakikishia atakuwa mwaminifu katika ndoa yake. Alimpenda sana mumewe ingawa hakuwa na pesa za kumtunza akapendeza vizuri, ndiye aliyempatia mumewe mtaji wa kufungua saluni baada ya kuwaomba wazazi wake fedha za biashara.
Je, nini kitaendelea? Usikose USIKOSE KESHO ASUBUHI…
Pia kitabu changu cha MAPENZI ASILIMIA 100% Kimetoka, kinauzwa madukani Kariakoo mtaa wa Muhonda. Kwa tsh 12,000/= tu. Pata nakala yako. 0674894889.

Na Zubagy Akilimia

Leave A Reply