The House of Favourite Newspapers

Chongolo Awapongeza Umoja Wa Wanawake Tanzania (Uwt)

0

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewapogeza Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuandikisha wanachama wapya, kuhimiza wanachama kulipa ada na kubuni miradi mbalimbali ya kiuchumi.

Katibu Mkuu ametoa pongezi hizo akiwa mgeni rasmi katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) lililofanyika leo tarehe 20 Disemba, 2021 Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma.

Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Maeneo hayo matatu kwa CCM ni muhimu sana, bila hayo hakuna Chama wala Jumuiya, kwani bila kuingiza wanachama wapya maana yake waliopo wataendelea kupungua, bila kuwa na msingi imara wa uchumi jumuiya itakuwa ombaomba na bila kujenga uhai wa jumuiya hatutakuwa na jumuiya imara na yenye nguvu ya kusimamia maslahi ya wanawake nchini.

Aidha, UWT kupitia kwa Mwenyekiti wake Taifa Ndg. Gaudensia Kabaka, imetoa tamko la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunda kamati maalum ya kumshauri kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia, ambapo itasaidia katika kufikia malengo ya hamsini kwa hamsini katika fursa mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Uwt Zanzibar Ndg. Thuwaiba Kisasi amesisitiza kuwa, wanawake wataendelea kusimama kidete katika kusimamia maslahi ya wanawake wote nchini na ya Chama Cha Mapinduzi.

Kikao hicho za kawaida, kimehudhuriwa pia na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akiwemo Katibu wa NEC, Oganaizesheni Ndg. Maudline Castico na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Dkt. Edmund Mndolwa.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Wakati tukielekea kufunga mwaka 2021, tunakumbuka matukio ya mauaji yaliyotokana na sababu mbalimbali.

Matukio hayo yalisababisha hofu miongoni mwa wanajamii huku sababu za matukio hayo zikitajwa kuwa ni ugomvi katika mapenzi, ulevi, ugomvi miongoni mwa ndugu na migogogo katika jamii.

Moja ya tukio lililotikisa mwaka 2021 ni lile lililotokea Agosti 25, 2021 ambako kijana Hamza Mohammed aliposabisha vifo vya watu wanne na wengine sita kujeruhiwa, kisha naye kuuawa na askari kwenye mapambano ya kurushiana risasi.

Tukio hilo lilitokea makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni jirani na Ubalozi wa Ufaransa, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Operesheni Maalumu Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas alipozungumza na waandishi wa habari alisema kati ya watu wanne waliofariki dunia watatu walikuwa askari polisi, huku mmoja akiwa mtumishi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA.

“Wakiwa kazini alikuja mtu mmoja akawashambulia askari hao kwa silaha ya aina ya bastola baada ya kuwashambulia na kuanguka alichukua bunduki zao mbili na kuanza kurusha risasi ovyo na kuelekea ubalozi wa Ufaransa. Alipofika hapo alijificha kwenye kibanda akawa anajihami huku akifyatua risasi ovyo,” alisema.

Lakini baada ya uchunguzi wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura alieleza walibaini kwamba Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Tukio lingine ni lile lililotokea Julai 16, saa 8 usiku maeneo ya kwa Mzungu-Mbezi Makabe wilayani Ubungo ambako Grace Mushi (25) alidaiwa kusababisha kifo cha aliyekuwa mpenzi wake Khamis Abdallah maarufu kama Zungu kwa kumchoma moto akiwa ndani ya nyumba.

Kamanda wa Kanda Maalumu, Jumanne Muliro alisema mtuhumiwa aliamka usiku na kumfungia ndani Khamis kisha kumwaga petroli na kuichoma moto nyumba hiyo kitendo kilichosababisha kifo cha mwanaume huyo.

Pia tukio la mama na binti zake wawili kuuliwa na kijana wao wa kazi kilihuzunisha na kutengeneze hofu ndani ya jamii.

Kwa mujibu wa Kamanda Muliro, mtuhumiwa wa mauaji hayo Shadrack Kapanga (34) alifanya kosa hilo Juni 9, 2021 eneo la Masaki Mtaa wa Maryknol baada ya kuwapiga kwa kitu kizito na kuwasababishia kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 11, 2021 eneo la Magomeni akiwa kwenye harakati za kutoroka baada ya kuwaua Emilly Mutaboyerwa ambaye ni mama na Damita (13) na Daniela Mutaboyerwa (15) huku akiwa na baadhi ya vitu alivyoviiba baada ya kufanya tukio hilo.

Imezoeleka kuwa baa ni sehemu ya watu kuburudika, lakini ilikuwa tofauti Julai 17,2021, saa 11 jioni baada ya Alex Korosso maarufu kwa jina la Simba aliyekuwa katika baa ya New Lemax iliopo Sinza kumuua Gift Mushi kwa kumpiga risasi kisha naye kujiua .

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai ilieleza kuwa ulevi ndio ilikuwa sababu iliyochangia mauaji hayo.

Mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa Gift Mushi aliyepigwa risasi alikumbwa na tukio hilo, baada ya kumshauri Alex Korosso ambaye alikuwa mhasibu wa chama cha waigizaji nchini (TDFAA) kuacha tabia ya kuwatishia watu kuwapiga risasi wakati wakipata kinywaji.

“Gift Mushi alipigwa risasi moja ya mguu, mbili za tumboni baada ya kumuona anaendelea kuangaika chini alienda kummalizia kwa kumpiga risasi tatu kichwani na baadaye kurudi kwenye kiti alichokaa kujimalizia mwenyewe kwa kujipiga risasi moja kichwani” alisema.

Wakati hayo yakitokea, Oktoba 11, mtendaji wa kata ya Msumi, Kelvin Mowo (38) aliuawa wakati akitekeleza majukumu yake katika ofisi za serikali za mitaa Mbezi Msumi.

Kwa mujibu Kamanda Muliro, marehemu akiwa ofisini kwake akisikiliza mgogoro wa ardhi ghafla watu wanne waliingia ofisini na mmoja akatoa panga na kumshambulia, kitendo kilichosababisha kupata majeraha makubwa na baadaye kupoteza maisha wakati akikimbizwa hospitali.

Matukio mengine

Oktoba 5, Mwenyekiti wa kijiji cha Kombo, Kata ya Kibosho Magharibi, wilayani Moshi, Joachim Sakaya aliuawa kwa kukatwa mapanga na kisha mwili wake kutupwa shambani.

Pia Septemba 26, mkazi wa kijiji cha Makami Juu, Kata ya Kilema Kaskazini wilayani Moshi, Gaspar Mremi (58) aliuawa na watu wanaodaiwa kukodiwa kwa Sh300,000 ili kulipiza kisasi kwa kumpiga baba yake.

Mei 31, askari polisi Linus Nzema wa kituo cha Polisi Mwanga aliuawa kwa kupigwa risasi nje ya baa iitwayo Ndafu iliyopo kijiji cha Kituri, baada ya kuzozana na askari mwenzake waliokuwa doria.

Mbali na hilo, Juni 2021, mlinzi wa Suma JKT, Emmanuel Mallya alidaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi akiwa lindo kituo cha kupooza umeme cha Kiyungi, mkoani Morogoro.

Julai 12, Mkazi wa kijiji cha Challa wilayani Rombo, John Kavishe (77) anadaiwa kumuua mwanaye Andrew Kavishe (31) kwa kumkata panga shingoni wakati akisuluhisha mgogoro wa kifamilia.

Pia Agosti 30, Elice Matafu mkazi wa kijiji cha Mrimbo Uwo, kata ya Mwika wilayani Moshi ambaye ni mke wa mfanyabiashara Patrice Matafu aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani.

Kauli ya wanasaikolojia

Mwanasaikolojia Charles Kalungu alisema kisaikolojia mtu hufanya kitendo cha kutisha kwa ampendae akiamini atapata nafuu ya maumivu anayoyapitia moyoni mwake baada ya kukosa suluhu.

“Inapotokea migogoro ya mara kwa mara katika uhusiano ambao huweza kusababishwa na mambo mbalimbali huzalisha hisia, kitaalamu huitwa projectional feelings, yaani kuhamishia maumivu kwa mtu asiye na hatia.

“Hali hii husababisha mtu kushindwa kuvumilia maumivu, hata mtu mpole huwa mkali na anaweza kufanya vitu vya ajabu pale maudhi yanapozidi,” alisema Kalungu.

Josephine Tesha ambaye pia ni mwanasaikolojia alisema mara nyingi matukio ya mauaji husababishwa na tamaa.

“Japokuwa maamuzi yetu mengi kama wanadamu huwa yanasukumwa na hisia, lakini hatuwezi kuhusisha maamuzi maovu moja kwa moja na hisia. Mpaka mtu anafikia uamuzi wa kuua inawezekana alikuwa akikabiliana na hisia mbaya.

“Kitu pekee ambacho kitafanya kosa hilo lisichukuliwe kwa uzito wake ni kama atafanyiwa uchunguzi na kuonekana ana magonjwa ya akili,” alisema Josephine.

Leave A Reply