The House of Favourite Newspapers

 Mabishano Kuhusu Sare za JWTZ Kesi ya Mbowe

0

MABISHANO ya kisheria yameendelea leo Jumatatu Desemba 20, 2021 katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu kati ya mawakili wa Jamhuri wanaotaka mahakama ipokee kama kielelezo cha sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na wale wa utetezi wanaopinga vikali.

 

Baada ya mabishano yalichukua takribani saa sita, Jaji Joachim Tiganga ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 10, 2022 ambapo atatolea uamuzi wa pingamizi hilo.

Soma hapa mabishano ya hoja za mawakili

Wakili Kidando: Tunaendelea kwa kusema kwamba pamoja na mawakili wasomi kuelezea baadhi vifungu ikiwemo PGO, 229 inazungumzia kuhusiana na utunzaji wa vielelezo polisi.

 

Wakili Kidando: Na katika PGO hiyo 4c inamtaka polisi pale anapoviondoa kuandika kwenye notebook.

Wakili Kidando: Katika ku support hoja zetu shahidi ameweza kueleza chain of Custody.

Wakili Kidando: Shahidi wetu ameweza kuonyesha vielelezo ambavyo ndiyo alivyovikamata.

Wakili Kidando: Tukirejea shauri la Mahakama ya Rufaa lililokuwa linamuhusu Kened Shayo na wenzake dhidi ya Jamuhuri iliyoketi Arusha.

 

Wakili Kidando: Jaji hoja yetu nyingine pamoja na wenzetu waliporejea gad line waliokuwa wakisisitiza chain of Custody.

Wakili Kidando: Pamoja na mapingamizi yote yaliyojikita kwenye chain of Custody tunaomba mahakama yako upande wa utetezi hakuna hata mmoja aliyeweza kuonyesha upekuzi haukufanyika kabisa.

Wakili Kidando: Naomba uone hoja zilizojikita kwenye chain of Custody hazina hoja kisheria naomba uzitupilie mbali.

 

Wakili Kidando: Shahidi wa 8 katika vielelezo alivyovileta mahakamani kuliibuka hoja iliyotolewa na wakili Nashon lakini pia Wakili Malya, Dickson na Kibatala

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba kujibu hoja hizo kwa pamoja

Wakili Kidando: Ni hoja zetu kwamba shahidi wa nane ni competent kutoa vielelezo hivi hapa mahakamani.

Wakili Kidando: Ni submission yetu kwamba kutoa vielelezo hivi sio hitaji la kisheria aonyeshe ujuzi wa utambuzi na wala hakutakiwa awe amewahi kufanya kazi JWTZ isipokuwa katika hatua ya kukamata hivyo vielelezo inatosha kutoa utambuzi kama aliivyoonyesha kwenye utambuzi wake.

 

Wakili Kidando: Katika ushahidi wake aliongozwa Kuelezea muonekano wa vielelezo hivyo ikiwemo muonekano na rangi

Wakili Kidando: Lakini pia alienda mbali kwa kuonyesha alama alizoziweka pamoja na alama nyingine zilizomwezesha kutambua.

Wakili Kidando: Katika hoja hiyo hakueleza ni muda gani aliweka lakini kwa kupitia mwenendo tumebaini alisema aliweka mara baada ya kuvikamata.

 

Wakili Kidando: Jaji Katika hilo eneo la competence iliibuka hoja ambayo vielelezo hivyo vinaweza kupatikana mahali popote na kwamba vilitakiwa zikaguliwa na JWTZ au JKT.

Wakili Kidando: Wakili Mallya alienda mbali kwa kufanya utambuzi wa vielelezo hivyo na kuna wakati alikosoa na kusema sare hizo sio za JWTZ ni za umoja wa Mataifa.

Wakili Kidando: Mawakili wasomi kwenye hoja hizi wamejielekeza vibaya kwa sababu zifuatazo

 

Wakili Kidando: Moja masuala waliyoibua hayawezi kutumika katika hatua hii kwa sababu mahakama katika hatua hii haipo kwenye nafasi ya kupima hayo waliyoibua yanatakiwa kuja kwa njia ushahidi

Wakili Kidando: Sababu ya pili wao kusema vielelezo hivi vinaweza kupatikana popote na wakili Malya kwenda mbali zaidi kwa kutofautisha kwa majina anayojua yeye

Wakili Kidando: Kwa mujibu wa sheria haina nafasi katika hatua hii na ni maneno ambayo hayana msaada kwa mahakama kama lilivyoibuliwa.

 

Wakili Kidando: Suala la competence ya shahidi ilishatolewa uwamuzi na Mahakama ya rufaa kwenye kesi Charles Gasirabo.

Wakili Kidando: Vigezo vilivyotajwa katika shauri hilo shahidi wetu ametimiza majukumu yake Agosti 8,2020 na ameshasema kwenye ushahidi wake.

Wakili Kidando: Kwenye kutambua vielelezo hivyo hapa mahakamani inadaiwa Shahidi hajaonyesha unique futures, katika maamuzi kadhaa yaliyotolewa hatujakutana na kitu kinachoitwa unique futures.

 

Wakili Kidando: Ni submission yetu kwamba shahidi ameonyesha unique futures hapa mahakamani…….

Wakili Kidando: Shahidi alienda mbali na kuonyesha alama aliyoiweka yeye

Wakili Kidando: Ni hoja yetu kwamba shahidi namba nane ameweza kuonyesha competence hapa mahakamani kwa kuonyesha alivyopita kuvishughukikia na kuonyesha utambuzi wake kwa vyeo vyake viwili vya unique futures

Wakili Kidando: Na kuomba kuvitoa kama sehemu ya ushahidi wake ameonyesha ni competency na vinaweza kupokelewa na mahakama hii.

 

Wakili Kidando: Tunaona hoja hazina mashiko na tunaomba uyatupilie mbali

Wakili Kidando: Hoja iliyotolewa na Wakili Kibatala akidai tumewashangaza kwa kuleta vielelezo hivi kinyume cha sheria

Wakili Kidando: Hoja hii haina mashiko kisheria kwasababu ushahidi huu sio mpya kama mawakili walivyodai na ushahidi uliokuwepo tangu yaliposomwa maelezo ya mashahidi na ukasomwa mahakamani.

Wakili Kidando: Wakati wa kusoma maelezo ya mashahidi tulieleza tutakuwa na vielelezo wakati wa usikilizwaji kile tulichotakiwa kufanya tulifanya kwa kufuata sheria

 

Wakili Kidando: Tulichotakiwa ambacho hata mahakama ilisisitiza tulisoma ushahidi wote ambao Jamuhuri walikuwa na nia ya kutumia.

Wakili Kidando: Kwa wakati haikuwa hitaji la kisheria la kuviorodhesha kwa mujibu wa uwamuzi wa mahakama hii ya mwaka 2006.

Wakili Kidando: Hivyo Mheshimiwa Jaji pamoja na Kibatala kufanya marejeo ya kesi na pamoja kuwa ni sheria inayobana mahakama hii shauri lile ni tofauti na mazingira ya kesi hii.

Wakili Kidando: Kwa sababu kuna kanuni ya nane ya maamuzi ya mahakama hii ni submission yetu kwamba hatuwezi kutumia kifungu cha 246 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai hivyo hoja hiyo haina mashiko kisheria tunaomba uitupilie mbali

 

Wakili Kidando: Tunaomba kwenda kwenye hoja nyingine Wakili Mallya aliomba vielelezo vinavyotakiwa kutolewa na shahidi visipokewe kwa kuwa kutolewa kwa not book kuna kitu kinachofichwa na shahidi

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji hoja hii tulizungumzia wakati tunajibu hoja ya kwanza ya wakili Nkungu ntaongeza vitu vichache.

Wakili Kidando: Shahidi aliieleza kwanini hajaleta hiyo not book na kwamba haihusiani na tuhuma alizokuwa anachunguza.

Wakili Kidando: Tumeomba kuirejesha mahakama katika maamuzi ya mahakama ya rufaa kwamba maelezo ya mawakili hayawezi kutumika kama ushahidi hivyo hayawezi kuamua.

Wakili Kidando: Hivyo hoja hii nayo tunaomba uitupilie mbali

 

Wakili Kidando: Pia hoja ya Wakili Mallya kwamba kidaftari na kwenye kusoma maelezo ya mashahidi hawakusema kama kulikuwa na karatasi iliyobanwa

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji utaratibu uliopo na unaofahamika na kupeleka shauri mahakama kuu Mkurugenzi wa Mashtaka hupeleka nyaraka zote ambazo zitabeba ushahidi na Jamuhuri watautumia wakati wa kesi.

Wakili Kidando: Katika mazingira hayo na kwa kuwa zoezi zima la kutoa ushahidi pamoja na vielelezo wakati wa Mwendelezo wa kesi katika Mahakama ya Kisutu ukurasa wa 233 kidaftari hicho kimeorodheshwa.

Wakili Kidando: Kwa mujibu wa nyaraka tulizopeleka na kwa utaratibu huwa tunatoa nakala kidaftari hicho na sisi tukiangalia kwenye nakala zetu hiyo sehemu yenye pini ilikuwa committed.

 

Wakili Kidando: Baada ya kuonyesha hivyo tunasema hiyo karatasi iliyobanwa na Iinafanya mawakili wasema haikuwa sehemu ya ushahidi inakosa mshiko. ……………….

Wakili Kidando: Point hiyo haiwezi kuzuia kupokewa kwa kielelezo ambacho shahidi ameomba kukitoa hapa mahakamani

Wakili Kidando: Naomba kwenda kwenye hoja nyingine iliyotolewa na Kibatala akidai kulikuwa na ukiukwaji wa PGO 229

 

Wakili Kidando: Ni hoja yetu kwamba PGO 229 ni muongozo unatumika katika upelelezi linapokuja suala la vielelezo hivyo kuchambuliwa kutofautishwa na kuwekwa alama.

Wakili Kidando: Vielelezo ambayo Shahidi wa nane ameomba kuvitoa mahakamani ameviweka alama na wakati wa kuviweka alama ni vielelezo vilivyo kamatwa na kuletwa mahakamani kwaajili ya kutoa ushahidi.

Wakili Kidando: Ni maoni yetu kwamba alama aliyoiweka shahidi wa nane inajitosheleza na ndio iliyotajwa kwenye ukurasa wa tatu.

 

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji kama tulivyotangulia kusema PGO, 229 haihusiani na badala yake kanuni za kisheria zimetoa mwongozo ambapo zikiangaliwa zimetimiza kanuni zote za kisheria kama alivyoonyesha shahidi wa nane.

Wakili Kidando: Tunaomba uone pingamizi hili halikidhi vigezo kisheria .

Wakili Kidando: Ni pingamizi la Kibatala aliposema shahidi wa nane hausiani na ushahidi wake kama ulivyo kwenye kilelezo namba 14 alisema amefanya upekuzi nyumbani kwa Bwire Yombo Kilakala lakini kwenye kielelezo kumeandikwa Temeke.

 

Wakili Kidando: Ushahidi wake unafanana uko wazi kabisa tangu anatoa ushahidi wake alisema alipata taarifa mshtakiwa wa kwanza ana makazi Temeke hadi walipopata taarifa na kufika huko kunakoitwa Kilakala

Wakili Kidando: Upekuzi ulifanyika mbele ya mashahidi na Shahidi anasema baada ya kumaliza alimrudisha mtuhumiwa kituo cha polisi Chang’ombe.

Wakili Kidando: Huyu shahidi wakati wa ushahidi wake hili eneo kilaka ni mtaa na anasema mmoja wa mashuhuda ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa

 

Wakili Kidando: Ukiangalia ushahidi wa shahidi wa nane hoja ya Wakili Kibatala inakosa mashiko kisheria.

Wakili Kidando: Unaweza kuangalia tuchukue mazingira ya eneo na akasema ichukue Kilakala ipo Morogoro

Wakili Kidando: Kama kuna Kilakala nyingine ipo Morogoro katika kifungu hiki tafsiri aliyoisema mwenzetu haiko sahihi na hoja aliyoitoa mwenzetu haina mashiko kisheria

Wakili Kidando: Tunaomba kwenda kwenye point nyingine Wakili Kibatala alisema PGO 226 (2) ilikiukwa mwenye mamlaka wa kuingia kwenye makazi kwaajili ya upekuzi ni Afisa na huo ndio utaratibu wa kwenda kufanya upekuzi

Wakili Kidando: Alisisitiza mara na baada kujulisha ni kitu gani kimepatikana kwenye upekuzi

 

Wakili Kidando: PGO hiyo imemtaja maofisa wanaoruhusiwa na shahidi wa nane tangu mwanzo alikuwa anasema alikuwa mmoja wapo wa Afisa wa Polisi hivyo upekuzi aliofanya ulikuwa unaruhusiwa kisheria pamoja na kwamba katika ushahidi wake hakuna sehemu alionyesha kwa Hakimu na kufanya hivyo hatuoni vielelezo hivi alivyokamata visipokewe mahakamani

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji Kibatala alidai PGO 229 imekiukwa kuhusiana na ni nani alikuwa na funguo za chumba kilichokuwa kunatunza vielelezo hivyo

Wakili Kidando: Shahidi ametoa ushahidi kuwa Joston ndie alikuwa anatunza vielelezo hivyo pale Central polisi

Wakili Kidando: Na katika ushahidi wake pia chini ya kiapo aliieleza kumkabidhi na ndiye aliyekuwa anavitunza hadi vilipoletwa mahakamani.

 

Wakili Kidando: Yale masharti yaliyoko kwenye PGO 229 hatuoni mahali popote ambapo hapajajitosheleza tunaona kabisa katika ushahidi wake ameeleza namna vilivyotunzwa hadi kuletwa mahakamani

Wakili Kidando: Katika hoja hiyo Kibatala alirejea maamuzi ambayo mahakama hii ilishayatoa kuhusiana kupokewa au kutopokewa kwa vielelezo

Wakili Kidando: Na utakapokuwa unatoa maamuzi unaweza kurejea maamuzi ambayo ulishayatoa.

Wakili Kidando: Kwa kumalizia tunaomba uone kwamba mapingamizi yote yaliyoletwa hayana mshiko kisheria na yanapaswa kutupiliwa mbali

Wakili Kidando: Naomba uone vielelezo hivi ambavyo shahidi wa nane amevileta vinaweza kupokewa. Vielelezo hivi ni matokeo ya kielelezo namba 14

 

Wakili Kidando: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

Wakili wa mshtakiwa wa kwanza Nashon Nkungu anaanza kusawazisha hoja zilizotolewa na upande wa Jamuhuri.

Nkungu: Mheshimiwa Jaji tumesikia majibu ya upande wa mashtaka naomba kupewa kesi zilizotumika ili niweze kujibu.

Nkungu: Wakili Kidando alisema tumeshindwa kuelewa matumizi ya PGO 229 tunasisitiza PGO iko sawa na inataka kielelezo kinapotoka mikononi kwa mtuhumiwa kwenda kwa polisi ionyeshe ni namna gani alikuwa anavitunza.

Nkungu: Sheria imeenda mbali zaidi inataka kuandika kwenye not book yake.

 

Nkungu: Hoja nyingine shahidi aliieleza alivyomkabidhi vielelezo Sajenti Johnstone hadi alipoenda kuvichukua lakini maneno tu hayatoshi hata yawe matamu kiasi gani.

Nkungu: Tunazidi kusisitiza rekodi inatakiwa iwepo ni namna gani vitu hivyo vilivyoamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyinge.

Nkungu: Hoja nyingine tuliyowasilisha ni kwamba vielelezo hivi vinapatikana kwenye kielelezo namba 14 na kwakuwa vitu hivi vilichukuliwa na mtu mmoja na vinamuhusu mshtakiwa tunaomba vielelezo hivi viletwe mahakamani vyote.

 

Nkungu: Shahidi anasema notebook haina umuhimu lakini sheria iko wazi kama tulivyoeleza zote zinaeleza ni namna gani vielezo vitahifadhiwa.

Nkungu: Hapa Shahidi aliona notebook hiyo hamsaidii lakini sheria inataka kama haitumiki basi irejeshwe kwa mwenyewe.

Nkungu: Mheshimiwa Jaji suala la chain of custody mtu anaweza kusema hili labda awe mgeni hapa mahakamani

Nkungu: Tulishalisema hapa ili kielelezo kiingie inataakiwa kiwe kimeonyesha chain of custody

Nkungu: Sheria inaelekeza lazima kielelezo kionyeshe pale kilipoanzia hadi kugonga mlango wa Mahakama

Nkungu: Shahidi alishaeleza hapa ni namna gani alipeleka kule mahakama kuu ingawa hakusema kwanini kilitolewa central hadi makao makuu

 

Nkungu: Wasiwasi wangu kielelelezo kilifikaje chumba cha mashtaka na hakusema alikiachaje pale na kwa muda gani.

Nkungu: Tuliona kwamba kielelezo kilifika mahakamani lakini sio kwa mkono wa shahidi huyo ndio wasiwasi wetu na haijaeleza.

Nkungu: Haiingi akilini kielelezo kinaweza kubadilika kirahisi kwanza hakina alama wala namba ya siri.

Nkungu: Ni vielelezo ambavyo ni vigumu kubadilika hoja zao hapa hazina mshiko yoyote

Nkungu: Mapema leo alivyoanza kueleza Wakili Kidando alisema PGO tulizoainisha haziendani lakini sheria iko wazi ukisema haziendani na PGO 229 lakini tulieleza ikiwemo polisi notebook

 

Nkungu: PGO inamuelekeza polisi kuwa na notebook mara zote kuna wakati angetakiwa kutoa maelezo kulingana na notebook hiyo.

Nkungu: Chain of Custody inatakiwa kuangaliwa pale nyaraka inapotakiwa kuingia mahakamani.

Nkungu: Upande wa mashtaka hawakufanya jukumu lao ili vielelezo hivi viweze kuingia mahakamani bila shaka yoyote.

Nkungu: Kama hakuna hata mmoja anaefahamu kama upekuzi ulifanyika hii sio hoja yetu

Nkungu: Sisi tulisema kuthibitisha kuleta nyaraka kama sheria inayosema.

Nkungu: Kuhusu competence hapa Wakili Kidando alisema sio lazima shahidi kuonyesha ujuzi

Nkungu: Kwa namna kesi hii ilivyo shahidi hajaonyesha ujuzi shahidi alisema nguo hizi ni za JWTZ na sisi tunasema ili shahidi ajue nguo hizo ni za JWTZ lazima awe na ujuzi.

 

Nkungu: Mheshimiwa Jaji nilieleza kifungu kilichotumika sio sahihi, vielelezo vilitoka kwenye mlolongo usiokuwa wa kisheria

Nkungu: Mheshimiwa Jaji tunaomba mahakama yako isichukue hoja za upande wa Jamuhuri kwa sababu

Nkungu: Kielelezo kipokewe na mahakama kinakomaza tabia za askari kuvunja sheria lakini pia mahakama iwe na haki ya wateja wetu kutofuatwa kwa sheria hizi mahakama ya rufaa imetengua hukumu nyingi kwa kueleza kuwa kuna baadhi ya sheria zilikiukwa.

Jaji. Tu break hadi saa nae

Kibatala: Bora tumalizie kwa kuwa sina hoja nyingi na Wakili Matata hayuko vizuri anaumwa hivyo hatakuwa na hoja.

Jaji: Upande wa Jamhuri mnasemaje

 

Wakili Kidando: Hatuna pingamizi

Wakili Dickson Matata na Wakili Gabriel wanaowatetea washtakiwa wa pili na watatu waliunga hoja za Wakili Nashon Nkungu.

Wakili wa mshtakiwa wa nne Peter Kibatala.

Wakili Kibatala: Tunaikumbusha mahakama shahidi huyu alienda mbali na kujivika uelewa JWTZ

Wakili Kibatala: Hapa anazungumzia vifaa vya JWTZ baada ya kupokea ushuhuda aliongozwa kutoa ushahidi na akasema ni nguo za JWTZ

Wakili Kibatala: Hakuonyesha ni kwa namna gani alifahamu hizo ni nguo za jeshi hakutuletea ushahidi ni kwa namna gani.

Wakili Kibatala: Tunarudi kama hakufuata maelekezo ya PGO 229 kuna suala halijajibiwa alisema aliweka alama ni kwa namna gani amefafanua

 

Wakili Kibatala: Ni nini kilichomfanya kuweka alama hizo na je aliweka mbele ya mashahidi?

Wakili Kibatala: Alisema alama hizo aliziweka baadae ni kwa namna gani mahakama itaamini ili iweze kuzipokea, kupitia kesi ya Charles Gazirabo haisaidii chochote.

Wakili Kibatala: Hatujawasiki wenzetu wakijibu PGO 8,9 na 10

Wakili Kibatala: Naomba niendelee kuhusina na maelezo ya mashahidi hakuna ubishi maombi haya kuwepo na kifungu hicho

Wakili Kibatala: Unapokuwa na vielelezo vya ziada vinatakiwa kufanyiwa maombi wametaja ukurasa wa 32 na 33 huoni sehemu iliyoandikwa JWTZ

 

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji wakati wa kuandika uwamuzi wako naomba usome hizo kurasa

wenzetu wanasema walitoa taarifa kuwa kuna vielelezo watavitoa baadae.

Wakili Kibatala: Tunaialika mahakama kufanya ulinganisho wa hivyo vitu viwili kama ni wakati wa kusoma maelezo ya mashahidi hawakuvitaja na kama walisoma lakin havikuainishwa.

Wakili Kibatala: Kuna ka point naomba ukatumie wakati unatoa uwamuzi wako kuna bastola ilikamatwa ni kwa nini imeainishwa tofauti wakati maelezo ya mashahidi.

Wakili Kibatala: Kuhusiana na ushahidi Shahidi mwenyewe anasema aliamua kuliondoa, lilisomwa wakati wa maelezo ya mashahidi.

Wakili Kibatala: Naomba rekodi zinikumbushe kama Wakili hakusema maneno haya

Wakili Kibatala: Kile kidaftari ambacho kilisomwa wakati wa maelezo ya mashadi kiliondolewa

Jaji: Unachozungumzia hapo ni kidaftari au Notebook

 

Wakili Kibata: Ngoja ni seme kitu ili kurahisisha

Wakili Kibatala: Hoja yetu hapa ni kwa nini vitu hivi viliondolewa kama vilisomwa wakati wa kusoma maelezo ya mashahidi.

Wakili Kibatala: Ukitaka kwenda kanisani basi u complain na masharti yaliyoko huwezi basi kaa nyumbani na hivyo ndiyo ilivyo.

Soma zaidi: Mawakili wa utetezi walivyombana shahidi kesi ya kina Mbowe

Wakili Kibatala: Katika uwasilishwaji wa vielelezo mahakamani shahidi alitakiwa kufuata sheria ya PGO

Kuhusu Kilakala hakuna maelezo yaliyotolewa upande mmoja kumetaja Yombo Kilakala na upande mwingi kumetaja Temeke.

Wakili Kibatala: PGO 229 inasema katika kuitunza vielelezo anaetakiwa kuitunza vielelezo ni OCS au Afisa mwingine atakaekuwa amechaguliwa

 

Wakili Kibatala: Shahidi anatuambia aliyekuwa anatunza ni Sajent Johnson sasa hajatumbia kama alikuwa ni askari wa kituo hicho au kituo kingine.

Wakili Kibatala: Ili kumlinda mshtakiwa Sheria inasema anatakiwa kulindwa na kulindwa kwenyewe ni kutombambikia kesi .

Wakili Kibatala kamaliza.

Jaji: Tumesikia hoja za pande zote mawakili mnaowatetea washtakiwa nawaomba ofisini.

Jaji: Baada ya mahakama kupokea hoja zilizowasilishwa tumekubaliana na mawakili wa pande zote mbili shauri hili iahirishwe hadi Januari 10,2022 washtakiwa wote wataendelea kuwa chini ya usimamizi wa Magereza hadi January 10,2022.

Leave A Reply