The House of Favourite Newspapers

Mastaa Afrika Mashariki watesa Kampeni ya Mali Safi Apple Music

0


MASTAA wa muziki katika Afrika Mashariki wamezindua kampeni inayokwenda kwa jina la Mali Safi inayoendeshwa na Kampuni ya Apple Music.

Lengo la kampeni hiyo ni kusherehekea muziki mzuri katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa wanamuziki waliofanya vizuri kwenye Apple Music.

Jumla ya wasanii kumi wamo kwenye orodha hiyo wakiwemo Diamond Platinumz, Zuchu, Navy Kenzo, Eddy Kenzo, Nandy (Tanzania), Sauti Sol (Kenya), Nikita Kering, Chris Kaiga, Spice Diana na Otile Brown.

Mali Safi ni silogani yenye maana ya kitu kizuri, kipya na chenye mvuto wa kipekee; Jambo ambalo wasanii wote waliopo kwenye kampeni hiyo wamefanikiwa kuwa nalo hapa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika kufanya uchaguzi bora, Apple Music itaweka nyimbo za wasanii maarufu, zenye ubora na zinazobamba zaidi kwa sasa na kisha kuzindua Mali Safi Kampeni, lengo likiwa ni kukidhi kiu ya wateja wa muziki mzuri Afrika Mashariki.

Hizi hapa chini ni baadhi ya kauli za wasanii hao waliopo kwenye kampeni hiyo.
 
“Muziki wa Afrika Mashariki ni chaguo la maisha ya watu. Muziki wetu unaonyesha utamaduni wetu ulimwenguni. Sisi ni onyesho kwa jamii tukisisitiza upendo na kuwakaribisha wengine kwetu,” – Sauti Sol.

“Tunaiunganisha jamii kwa mchanganyiko wa sauti mbalimbali za muziki kama Taarab, Genge, Bongo Flava na nyingine nyingi; na kila wimbo unajieleza wenyewe kwa mapigo yake,” – Navy Kenzo.

“Ni baraka kwa Afrika Mashariki kuwa na mastaa wengi wa muziki mbalimbali. Hii inatoa nafasi kwa wasanii kujaribu muziki wao kwa mashabiki wetu. Hivyo, kama unataka playlist nzuri zaidi, Afrika Mashariki pekee ndiyo mahali sahihi,” – Nikita Kering.

“Muunganiko wa muziki wenye hisia murua, na mashairi bora zaidi kutoka kwetu, ndiyo kunafanya muziki wa Afrika Mashariki kuwa bora zaidi hapa barani (Afrika)” – Nandy.

Na Mwandishi Wetu

Leave A Reply