The House of Favourite Newspapers

Chuchu Afungukia Kubuma 40 Ya Mwanaye

0
Staa wa Bongo, Chuchu Hans akiwa na mtoto wake.

 STORI: MAYASA MARIWATA | RISASI JUMAMOSI | HABARI

BAADA ya 40 ya mtoto wa mastaa wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray’, anayejulikana kwa jina la Jaden kudaiwa kubuma, mwanamama huyo amefunguka kuwa licha ya kuchelewa bado ipo na inakuja ‘soon’. Chuchu aliongea hayo baada ya habari kuenea kuwa mastaa hao wameshindwa kumfanyia mtoto wao sherehe ya kumtoa nje ‘40’ kutokana na hali ya kifedha kuwa mbaya kwao.

 

“Ni kweli tumechelewa kumfanyia 40 mtoto wetu lakini ‘soon’ itafanyika tu na haya yote yanatokana na maamuzi ya baba yake ndiye aliyepanga hivyo siyo kukosa pesa kama wanavyodai, siku ya shughuli ikikaribia utasikia fununu tu,” alisema Chuchu.

Leave A Reply