The House of Favourite Newspapers

Chuo Kikuu Ardhi Chafanya Utafiti Kudhibiti Matetemeko

0
Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakiingia kwa maandamano kwenye mahafali ya 14 ya chuo hicho yaliyofanyika Decemba 12, 2020 chuoni hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa chuo hicho ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Cleopa Msuya akimtunuku shahada ya uzamivu mmoja wa wahitimu wa shahada ya uzamivu kwenye mahafali ya 14 yaliyofanyika chuoni hapo Desemba 12, 2020.
Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni mwenyekiti wa Chuo Kikuu Ardhi Cleopa Msuya akitoka kwenye mahafali ya 14 ya chuo hicho.

 

CHUO Kikuu Ardhi (ARU) kimefanya utafiti kuhusu teknolojia ya asili ya ujenzi wa nyuba zinazostahimili matetemeko ya ardhi katika mji wa Dodoma  utakaowezesha kutumia taaluma hiyo kwenye ubunifu wa majengo ya kisasa ya mkoa huo.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa, ameyasema hayo jana, Desemba 12, 2010 wakati akizungumza kwenye mahafali  ya 14 ya chuo hicho ambapo wanafunzi 927 walitunukiwa shahada za awali, shahada za uzamili, shahada za uzamivu nne.

Amesema utafiti huo umefanyika kwa ufadhili wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na kwamba chuo pia kimesanifu na kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo jengo la Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma, Stendi Kuu ya Mabasi Mbezi Louis na usanifu wa uwanja wa kimataifa wa michezo utakaoanza kujengwa mkoani Dodoma hivi karibuni.

 

Profesa Liwa ameongeza (ARU), imebuni pia  teknolojia ya utengenezaji wa mkaa mbadala unaotokana na taka ngumu zikiwemo mabaki ya mazao ili kuongeza ujuzi na ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu na wakulima wadogo.

Amesema mradi huo umesaidia kupanga, kupima na kutoa hati miliki katika mji wa Mbarali na kupatikana kwa maeneo ya viwanda vidogo vidogo kwaajili ya utengenzaji wa mkaa na miundombinu kwaajili ya kusafirisha malighafi za viwanda hivyo.

Amezitaja fursa zingine zilizopatikana kuwa ni hati miliki na mitaji, kupunguza migogoro ya ardhi, kudhibiti magonjwa ya mlipuko na athari zitokanazo na tabia nchi.

 

Profesa Liwa amesema chuo pia kimefanya utafiti wa kuboresha matumizi na mbinu mpya za umwagiliaji katika bonde la mto Rufiji ili kuleta tija nan a kuongeza uzalishaji katika Wilaya ya Iringa pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za matumizi ya maji katika mto Rufiji.

Amesema mafanikio ya chuo hicho yasingewezekana kama siyo juhudi za pamoja baina ya chuo na wadau mbalimbali katika maendeleo ya sekta ya elimu wa ndani nje ya nchi.

 

Amewataja wadau hao kuwa ni serikali, SIDA ya Sweeden, GIZ na DAAD ya Ujerumani, Norway, Denmark na China huku akitambua mchango mkubwa wa wizara ya elimu sayansi na teknolojia katika kuendeleza na kutatua changamoto za chuo kikuu Ardhi (ARU) jambo ambalo limewezesha utoaji wa elimu bora na ukuaji wa taaluma.

 

“Kipekee niwapongeze wahitimu wote kwa hatua hii muhimu katika historia na maendeleo yenu binafsi na taifa kwa ujumla kwani natambua safari ya kufikia mafanikio haya haikuwa rahisi lakini juhudi kubwa na nidhamu ndiyo msingi wa mafanikio haya,” alisema

 

Amesema kwa mwaka wa masomo wa 2020/21 ARU imedahili wanafunzi 1,653 wa mwaka wa kwanza kwa shahada za awali na wanafunzi 97 kwa shahada za uzamili ikiwa ni ongezeko la asilimia nane ikilinganishwa na mwaka 2019/2020,

Amesema chuo kimeanzisha program mpya 13 za shaahda za awali, shahada za uzamili na shahada za uzamivu wakizingatia uhitaji wa soko la ajira na Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Leave A Reply