The House of Favourite Newspapers

Chuzi ndo hilo, hakuna kuonja! -23

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:

“Mh! Mbona ghafla sana Maua?”
“He! Jamani! Kwani nyie wanaume mna ghafla?”
JIACHIE MWENYEWE…

“Eee! Ratiba zikiingiliana ni ghafla tu.”
“Ina maana Benny huwezi kuua ratiba zako kwa mwaliko wangu mimi?”
“Kwani umenialika au umeniomba nije nikutembelee?”
“Haya, nakualika sasa. Leo naomba uje nyumbani kwangu.”
“Sawa, kuna siku nitakuja…”

“Mimi nataka uje leo bwana.”
“Mh! Maua bwana…nikisema ghafla ndiyo hupendi…oke, nitakuja leo.”
“Saa ngapi?”
“We unataka saa ngapi?”

“Mimi nataka ukitoka kazini nikufuate twende wote mguu kwa mkono.”
Baba Shua hakuwa na jinsi, alikubali…
“Basi nitakujulisha nikiwa natoka,” alisema.
“Sawasawa.”

Walipomaliza kupata chochote, walisimama wote, wakatoka huku Maua akiwa ametangulia mbele.
Baba Shua alishangaa sana kwa namna Maua alivyobadilika. Alikuwa akitembea kwa mwendo wa kujisikia, alinawiri, alinenepa kidogo na alitakata…

“Da! Huenda ningekuwa na Maua mambo yasingekuwa hivi yalivyo sasa na mama Shua. Halafu demu kapendeza ile mbaya, suruali imemkaa kama amezaliwa nayo,” alisema moyoni baba Shua huku mwili ukianza kumsisimka kwa kumfikiria Maua alivyo kwa siku zile na moyoni akawa anakumbuka zamani za mapenzi yao motomoto.
Nje, waliachana. Maua akaingia kwenye gari lake na kuendelea na safari zake lakini huku akimsisitiza baba Shua kumfuata baadaye, baba Shua alikubali akarudi kazini kwake huku akisema moyoni…

“Kumbe Maua ana gari! Aisee! Lakini huenda huyu Maua akanisaidia kunipunguzia stresi. Kama tutaishi kama zamani itakuwa poa sana. Naweza kuendelea na mama Shua kwa vile nimefunga naye ndoa lakini huyu Maua akawa ndiye chaguo langu.”

Kusema kweli kwa muda wa siku kadhaa nyuma za mshikemshike wake na mkewe mama Shua na Musa wake, siku hiyo baba Shua alijisikia ana amani sana baada ya kukutana na kipenzi chake Maua.
***
Kwa upande wake, Maua aliondoka naye barabarani akiwa na mawazo kibao kuhusu baba Shua…
“Naamini sasa Benny anajutia uamuzi wake wa kunimwaga mimi na kumchukua huyo malaya wake,” alisema moyoni Maua…akaendelea…
“Na safari hii nikimdaka, hachomoki, kweli kabisa.”
***
Saa kumi kamili ya alasiri, Maua alimpigia simu baba Shua…
“Mm…vipi Benny? Hujatoka tu?”
“Ndiyo natoka Maua.”
“Kwa hiyo?”
“Njoo basi twende.”

Maua alichoma mafuta mpaka ofisini kwa baba Shua, akamchukua kwenye gari lake mpaka nyumbani kwake.
Walishuka wote, wakatembea kwenda ndani huku Maua akiwatambulisha majirani kwa baba Shua…
“Jamani! Mama Kise, huyu anaitwa Benny…ni mchumba wangu. Alikuwa nje kwa masomo, sasa amerudi.”
“Oooo! Karibu sana,” majirani walimkaribisha baba Shua.

Kwa jinsi alivyo, mwonekano na mavazi, kweli baba Shua alionekana kufananafanana na mtu aliyetoka nje ya nchi.
Ndani, walifikia sebuleni. Maua alionekana mwenye furaha sana kwani walipofika tu sebuleni, alimbusu baba Shua kisha akampa denda la mbali sana, wakakaa…
“Karibu sana baby, hapa ndiyo kwangu…dada,” Maua alimkaribisha, akamuita msichana wa kazi…
“Abee dada…”
Msichana wa kazi alitokea kutoka uani…
“Msikilize mgeni anakunywa nini? Lakini acha tu, namjua huyu nitamhudumia mwenyewe,” alisema Maua akisimama na kwenda kwenye friji.
***
Ndani ya saa moja, Maua alimkaribisha baba Shua chumbani…
“Njoo upaone mahali anapolala ubavu wako,” alisema Maua.
Baba Shua akiwa ameshakunywa wine glasi mbili, hivyo amechangamka kidogo, alimfuata Maua kwa nyuma hadi chumbani…

“Da! Chumba kama cha waziri wa fedha,” alitania baba Shua, Maua akacheka.
Ni kweli kilikuwa chumba kizuri, kilichosheheni kila kinachohitajika kwa ajili ya chumba.
Kitanda cha kisasa kilichozibwa na godoro kubwa, kabati kubwa la nguo, redio yenye kutumia CD sita na kiyoyozi cha ndani kwa ndani, vyote hivyo vilikifanya chumba hicho kuvutia zaidi.
Baba Shua alifikia kujitupa na kunesanesa kidogo huku akimsifia Maua kwa kujitahidi kutengeneza maisha yake vizuri…

“Da! Umejitahidi sana baby wangu…hongera sana…”
“Asante sweet, lakini siku zile tukiwa bado wote uliweza kunipa njia ya namna ya kutumia fedha. Kwa hiyo kwa kutumia maelekezo yako nikawa nimejifunza jinsi ya kubana matumizi,” alisema Maua huku akiachia tabasamu laini na kumwangalia baba Shua.

Walizungumza mengi chumbani, mwishowe walijikuta wamejitupa wote kitandani. Walichezacheza wakiwa kwenye nguo, baadaye Maua alitoka kitandani na kwenda kufunga mlango kwa funguo…
“Kwarakacha…kwarakacha…kwacha!”

Msichana wa kazi aligunia moyoni. Kwake lilikuwa tukio geni sana kumwona bosi wake akiingia chumbani kwake na mwanaume. Hajawahi kuona!Simu ya baba Shua iliita, akaitupia macho na kuona jina la mke wake, akaipuuza…
“Baby mbona hupokei simu?” Maua alimuuliza…

Je, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Ijumaa katika Gazeti la Ijumaa.

Leave A Reply