The House of Favourite Newspapers

Common: Mabifu ya Wiki ya BET Huwa ya Kishamba Sana

0

 

MWANAMUZIKI mwenye jina kubwa, nguri, Common ameibuka na kutoa povu kwamba mabifu yanayotokea katika wiki za Tuzo za BET ni ya kitoto mno, tena ya miaka ya tisini.

Huku akionekana kumaindi ile kinomanoma, Common alionekana kumaindi zaidi kwani ugomvi uliotokea mtaani wa wanamuziki Meek Mil na Safaree hakika haukutakiwa kutokea kwani ulikuwa ni muda wa amani na kufurahia tuzo.

“Ni mabifu za kizamani sana, ni sawa na kumuona mtu siku hizi akivaa jinsi za Fubu au Jnco. Wasanii waache ushamba, Amani itawale na waache kupigana kwa vitu visivyokuwa na msingi,” alisema Common ambaye alikuwa ndani ya ndinga moja kali, Range SUV na baada ya kutoa povu lake, huyo akasepa zake.

Ikumbukwe kwamba chanzo kikubwa cha wawili hao kuingia kwenye bifu ni mwanamuziki Nicki Minaj ambaye aliwahi kutoka na wote wawili kitu kilichosababisha msuguano mkubwa.

Na: Nyemo Chilongani, (GPL)

Leave A Reply