The House of Favourite Newspapers

#GloblaNewsUpdates: Malinzi, Mwesigwa na Kaburu Wafikishwa Kortini

0

 

Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwasili mahamani Kisutu

 

 

Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa akiwasili mahamani Kisutu
 Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Rais wa Klabu hiyo Evans Aveva wakiwasili mahamani Kisutu

 

Aveva akiwasili

 

#GloblaUpdates: Hatimaye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Rais wa TFF, Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wake Celestine Mwesigwa, Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva, Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ pamoja na anayedaiwa kuwa ni Mhasibu wa Simba ambaye jina lake halijafahamaika kujibu tuhuma zinazowakabili.

TAKUKURU imekataa kuwaruhusu viongozi hao wa TFF wanaoshikiliwa kwenda kwenye usahili wa wagombea unaoanza leo. Viongozi hao ni wagombea walioomba ridhaa ya kutetea nafasi zao.

Aidha, TAKUKURU pia imekataa kumruhusu Kiongozi wa Simba Godfrey Nyange(Kaburu) kwenda kushiriki usahili wa wagombea TFF.

Ikumbukwe kuwa, Evance Aveva pamoja na Kaburu nao pia wanashikiliwa na TAKUKURU kwa tuhuma za kujipatia Fedha kwa njia yabudanganyifu wakati walipomuuza Mchezaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi.

Updates

Rais wa Simba Evansi Aveva na Makamu wake Kaburu wametuhumiwa kwa makosa matano yasiyo na dhamana. Kesi yao itasikilizwa tena Julai 13, 2017.

 

TETESI: Malinzi ahojiwa na TAKUKURU kwa matumizi ya zaidi ya Tsh. Bilioni 1.5 ya fedha za wadhamini bila kufata utaratibu.

Jamal Malinzi na wenzanke walivyowasili mahakamani hapo.

 

 

UPDATE: Malinzi, Mwesigwa na Nsiana wamesomewa mashtaka 28

Kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa EXCOM imeridhia kubadilishwa kwa Signatories wa Bank hii inamhusu Malinzi na Mwesigwa pia.

Kufoji risiti za kuwa Malinzi anaidai TFF (risiti zipo zaidi 20 zinazodaiwa kufojiwa) hii inamhusu Malinzi pekee.

Na Mwisho ni shtaka la kutakatisha fedha dola za kimarekani 375418 hii inamhusu Malinzi, Mwesigwa na Nsiana

Leave A Reply