The House of Favourite Newspapers

Kimini Cha Kajala Chazua Gumzo Ukumbini

0
Staa mtata katika kinu cha ‘kutwangia’ filamu Bongo, Kajala Masanja.

AMEYAZUA tena! Staa mtata katika kinu cha ‘kutwangia’ filamu Bongo, Kajala Masanja, ambaye kama utasumbuka kumtambua kwa jina hilo, mtaje kwa ufupi wa Mama Paula, amerudi tena na awamu hii amezua gumzo kwa kuteka akili za watu, hususan wanaume wakware, kufutia kutinga kinguo kifupi ‘mini-sketi’ ukumbuni, hali iliyoibua viulizo na maswali kibao, teremsha macho hapa chini.

Ilikuwa Jumatatu, siku ya Eid-mosi ndani ya Ukumbi wa King Somolon uliopo Namanga jijini Dar, ambako pamoja na shamrashamra zingine, kulikuwa na shoo ya kukatika shoka na mpini kubaki, ikiwakusanya wasanii wa vichekesho kutoka nchi za Tanzania, Kenya na Uganda iliyoitwa jina la Eid-Comedy Gala, huku Kajala akiwa miongoni mwa wahudhuriaji wa mtanange huo.


Awali, ‘kiranja’ wa mtandao huu namba moja kwa habari za mastaa Bongo, aliyekuwa ameweka kambi nje kidogo ya ukumbi huo alimshuhudia msanii huyo aliyekuwa kimya kwa muda mrefu sasa, akiingia ndani sanjari na kampani na watu wake wa karibu akiwemo mwanaye Paula ambaye akikaa mbali na mama yake, huku Kajala akichagua viti vya mbele.

Kajala na mwanaye Paula

Miguno, mishangao, viulizo na maswali vilianza kurindima chini kwa chini ukumbini humo, baada ya Kajala kukaa na ‘kisketi’ chake kupanda juu zaidi kutokana na ufupi wake, hivyo kuacha wazi sehemu kubwa ya mapaja yake huku akijaribu kutumia mkoba wake kuzibaziba hali iliyolazimisha macho ya wengi kuweka kambi juu ya eneo hilo nyeti la mwili wake.

Paula katika pozi

“Aaaah, jamani hii sasa ni too much, huyu msanii mbona habadiliki tu? Hivi haoni kama umri wake umekwenda na ukitazama mwanaye ameshakuwa binti mkubwa, hadi avae mavazi yanayoacha wazi sehemu nyeti kama mapaja? Aibu gani hii jamani? Ona sasa watu wanavyomshangaa!” walisikika baadhi ya watu waliokuwa wamekaa karibu na mwandishi wetu, wakijadili uvaaji huo wa kihasara wa msanii huyo.

Kwa upande wake, licha ya macho ya wengi kumtazama mfululizo, Kajala hakuonekana kujali hali hiyo na badala yake alijikita zaidi kufuatilia vichekesho vilivyokuwa vikiangushwa jukwaani na wasanii hao ‘alwatani’ katika eneo la uchekeshaji na mwandishi wetu alimkaribia na kumuuliza kuhusu kinguo chake ambapo alipotezea kiaina kama maswali ya mwandishi hayakumhusu yeye.


Shoo hiyo ilipambwa na wacheshaji Eric Omondi (Kenya), Teacher Mpare (Mpare) na Kundi la Wasakatonge likiundwa na wasanii MC Pilipili, Katarina wa Karatu, Mau Fundi na Dogo Mapepe.

(Stori: Brighton Masalu / GPL)

Leave A Reply