Kartra

Conte Aachana na Inter Milan

MABINGWA wa Italia klabu ya Inter Milan italazimika kumlipa Antonio Conte kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni 19.8 kama fidia baada ya kusitisha mkataba.

 

Conte na Inter wamefikia makubaliano ya kusitisha mkataba baada ya kutofautiana kwenye usajili kwenye timu hiyo, anaondoka kwenye Klabu hiyo akiwa amewapa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu ya Italia (Escudetto) baada ya miaka 11.

Inter Milan walitaka kuuza wachezaji kutokana na changamoto za kiuchumi huku Conte akitaka aongezewe wachezaji ili awanie ubingwa tena wa ligi na Ligi ya Mabingwa (Uefa).


Toa comment