The House of Favourite Newspapers

Corona Kenya: Mtoto Miaka 6 Afariki, Walioathirika Wafikia 122

0

IDADI ya wagonjwa wa virusi vya corona (Covid-19) nchini Kenya imefikia 122 baada ya watu wengine 12 kuthibitishwa kuwa navyo ndani ya saa 24 zilizopita.

 

Katibu wa kudumu katika Wizara ya Afya, Mercy Mwangangi, amesema kwamba kati ya raia hao waliopatikana na virusi hivyo ni Wakenya 11 na raia mmoja wa Somalia.

 

Aidha amesema kwamba Kenya imepoteza mgonjwa mwengine kupitia virusi hivyo na kufanya idadi ya waliofariki kufikia wanne akiongeza kwamba mgonjwa huyo ni mvulana wa miaka sita ambaye alikuwa akiugua ugonjwa uliokuwa ukiathiri kinga yake.

 

Siku ya Alhamisi Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe, alisema kwamba watu wengine wawili walipoteza maisha yao kutokana na maambukizi ya virusi hivyo na kwamba  idadi hiyo inaongeza idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia watatu.

 

Kagwe ameongezea kwamba wagonjwa waliofariki wanatoka miji ya Nairobi na Mombasa.

Leave A Reply