The House of Favourite Newspapers

Corona: Miili ya Waafrika Itatapakaa Mitaani – Melinda Gates

0

MELINDA GATES, mke wa bilionea Bill Gates wa Marekani, ameonya kwamba iwapo dunia haitachukua hatua  za haraka za kukabiliana na janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, maiti za Waafrika zitatapakaa katika mitaa ya Afrika.

Bi Gates ametoa onyo hilo akizungumza na shirika la habari la  CNN la Marekani, kuhusu athari kubwa itakayozikumba nchi maskini duniani.

Alisema moyo wake uko Afrika na kwamba ana wasiwasi mkubwa kwamba bara hilo huenda likashindwa kukabili madhara makubwa ya virusi hivyo.

“Litakuwa janga la kutisha katika nchi zinazoendelea.  Baadhi ya sababu zinazoonyesha kwamba idadi haijafikia hali mbaya, ni kwa watu wengi hawapimwi.

“Kinachotokea Ecuador ni kwamba miili inatupwa mitaani.  Jambo hili litatokea katika nchi za Afrika,” amesema mwanamke huyo.

Melinda ambaye ni mwenyekiti-mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates, ana wasiwasi hali itakuwa mbaya zaidi barani Afrika kutokana na mifumo duni ya tiba na ukosefu wa misaada ya kibinadamu.

Kwa mujibu wake, kitu muhimu alichokishuhudia ni pale China ilipoamua kuwaweka watu wake wengi chini ya karantini.

Aliongeza kwamba amewahi kutembelea miji na vitongoji vingi maskini barani Afrika na akajiuliza ni vipi watu wa bara hilo  watalikabili janga hili?  Kwani si rahisi kuishi katika mazingira ya usafi na afya katika maeneo hayo.

 

Leave A Reply