The House of Favourite Newspapers

Pierre Liquid Aambukizwa Corona, Alazwa Amana

0

MCHEKESHAJI Peter Mollel maarufu kama Pierre Liquid,  amebainika kuwa na maambukizi ya #COVID19 na sasa yupo Hospitali ya Amana akiendelea na matibabu.

 

Katika mahojiano, amesema:  “Nina bosi wangu wa karibu ambaye kapata ugonjwa huu na kwa kuwa mara nyingi tuko naye,  alinishauri na mimi nikapime kwa nia njema ili kama ninao nipate matibabu mapema na kuepuka kuwaambukiza wengine.”

 

Ameongeza: “Nilienda hospitali ya Temeke, wakanipima ndipo nilipokutwa ninao na kuletwa hapa Amana ambapo kwa sasa ni moja ya vituo vya wagonjwa.”

 

Hata hivyo, amesema kuwa yeye anahisi atakuwa ameambukiziwa baa maana ndiyo maeneo yake ya kujidai na hivyo amewapongeza baadhi ya viongozi waliotoa tamko la kufungwa kwa baa akisema ni hatua nzuri.

 

Amesisitiza kuwa maeneo ya baa watu kuwa makini kujikinga na ugonjwa huu ni ngumu na pia huhusisha mikusanyiko ambapo mtu akiwa hajalewa anaweza kukaa mbali na watu lakini pombe zikishamwingia, akili hiyo huwa haipo tena.

CREDIT: JF

 

Leave A Reply