The House of Favourite Newspapers

Corona Uganda: Madereva wa Malori Hakuna Kulala Hotelini

0

RAIS Yoweri Museveni ametangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na #COVID19.

 

Amesema hatua zaidi ni pamoja na kila lori kuwa na mtu mmoja yaani dereva peke yake ambaye hataruhusiwa kulala hotelini wala nyumbani kwa watu akiwa Uganda na mienendo ya madereva hao itachunguzwa.

 

Ameongeza kwamba kusitisha usafirishaji wa bidhaa itakuwa na athari kubwa lakini madereva hao ni tishio katika mapambano ya nchi hiyo dhidi ya #COVID-19 huku akitoa mfano wa janga la ukimwi kwa miaka ya 1980 na 1990 ambapo madereva wa malori walisambaza virusi vya ukimwi (VVU) kila walipopita.

 

Mataifa ya Uganda na Kenya yamekuwa yakiwafanyia vipimo vya #CoronaVirus madereva wa malori katika mipaka yao, hali iliyosababisha foleni ndefu ya magari hayo.

 

Njia ya usafirishaji mizigo kutoka bandari ya Mombasa nchini Kenya ni muhimu katika usafirishaji wa bidhaa muhimu kama vile chakula na dawa hadi Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Leave A Reply