The House of Favourite Newspapers

Simba Yamwekea Mtego Molinga

0

JINA la mshambuliaji wa Yanga raia wa DR Congo, David Molinga limeingia kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na Simba katika kuelekea usajili wa msimu ujao 2020/ 2021, lakini kukiwa na mtego mkali.

 

Molinga ndiye mshambuliaji anayeongoza kwa idadi kubwa ya mabao ndani ya Yanga akiwa amefunga mabao nane kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

 

Mkongomani huyo alijiunga na Yanga kwenye msimu huu akisaini mkataba wa mwaka mmoja ambao unamalizika baada ya ligi kumalizika, hivyo ni mchezaji anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine itakayomuhitaji.Hata hivyo, Simba wameweka mtego na wanachosubiri wao ni kuona Yanga wanaachana kabisa na mchezaji huyo ndiyo wamzoe jumla bila kuleta mgogoro wa pande mbili.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, mabosi wa Simba wanaamini Molinga ni straika mzuri mwenye uwezo wa kufunga mabao na kama akitua hapo basi atakuwa na msaada mkubwa kwenye timu hiyo akisaidiana na Meddie Kagere.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Molinga kama kiwango chake kingekuwa kidogo, basi asingefunga idadi hiyo ya mabao akiwa na Yanga na wanaamini kilichomkwamisha kutofunga mabao mengi zaidi alikuwa hajacheza muda mrefu.

 

“Kuna watu Simba wana imani kubwa na Molinga, wakiamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kufunga idadi kubwa ya mabao kama akijiunga na timu hiyo, kwenye msimu ujao.

 

“Ingawa kumekuwa na mabishano makubwa, wengine wanaamini kuwa kwenye kipindi hiki siyo sahihi kumfikiria mchezaji kama Molinga, lakini wengine wanakuja na hoja za msingi.

 

“Mmoja anasema kwanza hatakuwa na gharama kubwa kwa kuwa mkataba wake na Yanga utakuwa umekwisha, lakini anasema pia kuwa kama aliweza kufunga idadi ya mabao nane kwenye kikosi cha Yanga mwanzoni tu, hebu tuseme kwetu ukiachana na Kagere nani amefunga idadi hiyo ya mabao?

 

“Kuna maswali ambayo wakati mwingine yanawafanya watu wafikirie, lakini ishu hapa ni baada ya Yanga kumuacha kabisa, ndiyo Simba wanaweza kufikiri moja kwa moja kumchukua,”alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mshambuliaji huyo alijiunga na Yanga akitokea DC Motema Pembe ya Congo na alitua akiwa na uzito mkubwa ambapo alitumia kipindi cha maandalizi ya msimu kujiweka fiti kwanza.

Leave A Reply