The House of Favourite Newspapers

#Coronavirus Uganda: Idadi ya Wagonjwa Yafikia 9

0


UGANDA imethibitisha kuwepo wagonjwa tisa waliokumbwa na virusi vya Corona nchini humo kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Dr Jan Ruth Aceng, wakiwa ni rais wa nchi hiyo waliokuwa Dubai.  Amesema pia watu wote waliokutana nao wanatafutwa.

 

Alisema Dubai haikuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa zinachukuliwa kuwa na hatari hiyo kwa Uganda, na kwamba kwa sasa wanaona msimamo huo haukuwa sawa kwani wagonjwa wote nchini humo wametokea Dubai ambao walisafiri kwa ndege za mashirika ya Emirates au Ethiopia.

 

Pia alisema mgonjwa wa kwanza aliyegundulika na ugonjwa huo Jumamosi iliyopita anaendelea vizuri.

 

Naye Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, akizungumza na taifa hilo baada ya mgonjwa wa kwanza kugundulika Jumamosi, alitangaza kufungwa kwa safari zote za watu kuingia humo kutoka nje, kufungwa kwa safari za kimataifa za ndege na kufungwa mipaka ya nchi hiyo.

 

Amesisitiza pia watu kukaa mbali kwa mita nne kati ya mtu na mtu ili kuepuka kuambukizana virusi hivyo, na amewaomba wananchi kuepuka usafiri wa watu wengi kwa pamoja ili kupambana na hali hiyo

Leave A Reply