The House of Favourite Newspapers

Corona Afrika Kusini: Nchi Nzima Yawekwa Karantini kwa Siku 21

0

RAIS wa Afrika Kusini, Cyrill Ramaphosa,  ametangaza siku 21 za wananchi wote wa nchi hiyo kujifungia ndani ilikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona ambavyo mpaka sasa vimeathiri watu zaidi ya 400 nchini humo.

Ramaphosa amesema wakati wa mpango huo ambao unatarajiwa kumalizika Aprili 16 hakuna mtu ataruhusiwa kutokana nyumbani na watakosimamia jambo hilo ni idara ya maafa ya nchi hiyo.

Amesema katazo hilo la watu kutoka ndani halitawahusu watu wa idara ya majanga, polisi na watumishi wa afya ambao watakuwa wakiwazungukiwa wananchi kuwapatia mahitaji muhimu ambayo ni pamoja na chakula.

“Tusipochukua hatua hii sasa wagonjwa wataendelea kuongezeka na hatua hii inaweza kuwa na athari zake kiuchumi lakini tusipoichukua sasa athari zitakuwa ni kubwa zaidi, uamzi huu utaokoa maisha ya maelfu,” amesema Ramaphosa.

Leave A Reply