The House of Favourite Newspapers

Coutinho aaga Yanga, aitaja Simba SC

0

ANDREYCOUTINHO

Kiungo Mbrazili wa Yanga, Andrey Coutinho.

Nicodemus Jonas,Dar es Salaam
KIROHO safi! Kiungo Mbrazili wa Yanga, Andrey Coutinho, kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu hatima yake ndani ya Jangwani na kusema kuwa kwa hali ya mambo ilivyo, kwa vyovyote itakavyokuwa hawezi kubaki.

Hata hivyo, kiungo huyo amesema yupo tayari kucheza timu yoyote ya ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwemo Simba.

Nyota huyo pamoja na kukubalika kwa mashabiki na baadhi ya viongozi kutokana na uwezo wake wa kumudu wingi ya kushoto na mipira iliyokufa, hata hivyo amekosa nafasi ya kudumu kwa siku za hivi karibuni.

Mbrazili huyo ambaye aliletwa nchini na Marcio Maximo, ameliambia Championi Jumatano kuwa kwa maisha anayoishi kwa sasa Jangwani, dhahiri shahiri hawezi kubaki hata kama watataka aendelee.

“Kiukweli siridhishwi na maisha ninayoishi kwa sasa. Hata kama angekuwa mchezaji gani, kwa jinsi ninavyoishi hawezi kuridhika nayo. Siwezi kuongeza mkataba kwa hali ilivyo.

“Lakini nitakuwa tayari kubaki huku iwapo kutakuwa na timu yenye kunihitaji hata kama ni wapinzani wetu Simba, ila kama nitaona kimya naondoka kwenda nyumbani kwetu Brazil,” alisema kiungo huyo.
Mbrazili huyo mwishoni mwa msimu huu, atamaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga.

Leave A Reply