The House of Favourite Newspapers

Madai! Nadharia ya Corona Ilikoanzia na Aliyeisambaza

0

WAKATI janga la ugonjwa wa COVID-19 likiitingisha dunia, kuwekuwepo na nadharia na uvumi mbalimbali kutokana na kuibuka kwake.

 

Miongoni mwa uvumi na tetesi kuhusiana na ugonjwa huo ni kwamba virusi vya ugonjwa huo vilianzia katika maabara nchini China na kuishia mitaani hadi kusambaa duniani kote.

 

Nadharia hiyo inatokana na ukweli kwamba janga hilo lilianzia katika jiji la Wuhan nchini China ambako kuna taasisi mbalimbali za utafiti, ikiwa ni pamoja na utafiti wa ndege aina ya popo.  Kwa maoni hayo, inaaminika kwamba virusi hivyo “vilitoroka” kutoka katika maabara na kuingia mitaani.

Kuna madai mengine ambayo yanasema Covid “haukutoroka” tu kutoka maabara bali ulitengenezwa makusudi na wanasayansi wa China kama silaha ya kibaiolojia.

 

Covid-19 imetengenezwa maabara

Kwa mujibu wa taasisi ya Pew Research, karibu katika Wamarekani watatu kati ya kumi wanaamini kwamba Covid-19 ulitengenezwa katika maabara, ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya.   Asilimia 23 ya waliohojiwa wanaamini ulitengenezwa makusudi na asilimia 6 wakiamini ni kwa bahati mbaya.

 

Marekani Ilipeleka Covid-19 China

Kuna nadharia pia inayodai kwamba jeshi la Marekani liliupeleka ugonjwa huo nchini China. Kuna madai mbalimbali yaliyowahi kutolewa na mamlaka za China kwamba Marekani ilipandikiza ugonjwa huo China wakati wa Michezo ya Kijeshi Duniani ya Mwaka 2019 iliyofanyika Wuhan mwezi Oktoba.

 

Nadharia nyingine imeelekezwa katika utafiti wa mbegu za uhandisi jeni (GMO) ambao unadaiwa unaweza  kuvuruga mienendo ya jeni na kuruhusu virusi mbalimbali kuongezeka kutokana na kutokuwepo kwa uwiano wa kimazingira.

Wanaharakati dhidi ya GMO wamelaumu shughuli za kilimo cha kisasa ambacho husababisha virusi mbalimbali kuingia kwa binadamu kama vile Ebola, VVU na vingine.

 

Kitu cha kushangaza, kwa mujibu wa wataalam  ni kwamba mfumo wa GMO unaweza kuwa sehemu ya chanjo itakayopatikana.  Iwapo mradi wowote kati ya 70 ya kutafuta chanjo ukifanikiwa, hiyo itakuwa ndiyo njia pekee ya ulimwengu kujiondoa katika janga la Covid-19.

 

Wataalam wanasema chanjo ikipatikana lazima ifuate utaalam na mfumo wa GMO kama unavyotumika katika mimea, na hilo lilifanikiwa ndipo walimwengu wataacha kuliona neno GMO kuwa linaleta taswira chafu kwa binadamu.

 

 

Covid-19 haipo!

Wana-nadharia kama David Icke na Alex Jones wa Marekani, wanasema Covid-19 ni kitu ambacho hakipo, bali ni njama za tabaka la juu la watu ulimwengu zilizopangwa ili kuwanyima watu uhuru wao.

 

Wanadai hizo ni njama za kisiasa tu, kwani virusi vya corona “havina lolote zaidi ya mafua” na ndiyo maana wanasiasa hao wanaitumia dhana hiyo ili kuwachochea watu kufanya maandamano ya kukataa kufungiwa majumbani mwao katika majimbo mbalimbali nchini Marekani.

Sakata la 5G

Inasemekana virusi hivyo baada ya kutengenezwa, vilianza kusambazwa kwa njia ya umeme wa sumaku (electromagnetic) na chembechembe za kibiolojia za nyuklia ya tindikali (nuclear acid).

 

Lakini pia inadaiwa kuwa kusambaa kwa ugonjwa huu kumechagizwa na uvumbuzi wa teknolojia ya 5G na kwamba umekuwa ukisafirishwa kwa njia mionzi ya umeme wa sumaku (electromagnetic radiation) kupitia simu za mkononi. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa mtandao wa simu hauna uwezo wa kupitisha virusi.

 

Bill Gates Anahusika

Bilionea wa Dunia, Bill Gate amehusishwa huku video moja aliyofanya na Mtandao wa TED mwaka 2015 ikimwonyesha akizungumzia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola na kuonya kuwa kuna ugonjwa mkubwa utakuja wa virusi ambao utaangamiza maelfu ya watu duniani.

 

Jambo hilo limechagizwa pia na hatua ya Gates kutaka chanjo ya corona ipandikizwe kwa njia ya microchip ambayo itafuatilia mienendo ya binadamu.

 

Njama za wauza madawa

Wakati janga hilo likiendelea, kuna madai kwamba kuibuka kwa Covid-19 ni mipango ya wafanyabiashara wakubwa wa madawa ambao walipanga janga hilo ili kunufaika na biashara ya kuponya ugonjwa huo pindi ukitokea.

 

Inasemekana kwamba wauza madawa hao wakubwa ndiyo kwa sasa wapinzani wakubwa wa hatua za kuelekea kupatikana kwa chanjo ya ugonjwa huo duniani.

 

Naye Dkt. Annie Bukacek wa Marekani, anaendeleza nadharia ya kupinga watu kufungiwa majumbani mwao akisema kwamba idadi za vifo vinavyotokana na Covid-19 zinakuzwa tu ili kuwawekea watu karantini za kubakia majumbani mwao  na kuwanyima fursa za kujumuika kwa karibu.

Leave A Reply