The House of Favourite Newspapers

Curry Agoma Kwenda Ikulu ya Trump

0
Mchezaji wa Golden State Warriors, Stephen Curry.

MCHEZAJI wa Golden State Warriors, Stephen Curry amesema kama timu hiyo itaalikwa kwenye Ikulu ya Marekani (White House), baada ya kutwaa ubingwa wa NBA, yeye hatakwenda.

Kumekuwa na utaratibu wa muda mrefu kwa timu kualikuwa kwenye Ikulu ya Marekani kila inapotwaa ubingwa wa NBA na sasa kumekuwa na mgawanyiko mkubwa kuhusu urais wa Donald Trump wa nchi hiyo ambao umekuwa ukipingwa na raia wengi.

“Kuna mtu aliwahi kuniuliza miezi kadhaa nyuma, kama tutatwaa ubingwa wa NBA nitakwenda Ikulu? Nilimjibu kuwa sitakwenda na hivyo ndivyo ninavyojisikia leo,” alisema Curry.

Leave A Reply