The House of Favourite Newspapers

Obama Amtumia Ujumbe Kevin Durant

0
Kevin Durant

MARA baada ya kushinda taji la NBA, Jumanne ya wiki hii, akiwa na timu yake Golden State Warriors, staa wa msimu huu, Kevin Durant, simu yake ilikuwa bize akipokea meseji za pongezi lakini meseji moja ilitoka kwa rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama.

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama.

Durant ni kati ya wachezaji ambao walifanya kazi kubwa kwenye NBA msimu huu akimaliza kwa kuwa MVP na juzi alisema kuwa ujumbe mmoja wa pongezi ulitoka kwa Obama.

Anasema Obama alimtumia meseji kumpongeza kwa yeye kutwaa ubingwa huo wa kwanza wa NBA lakini aliipongeza timu yao yote. “Obama alitu- ma meseji ya pongezi kwetu na meseji yake ilisomekana hivi: “‘Hongereni. Safu yenu ya ulinzi ilikuwa imara sana, endeleeni kufurahia.” “Hata hivyo mimi sikutegemea kitu kama hicho, haya ni mafanikio makubwa sana kwetu,” alisema Durant

LOS ANGELES, Marekani

Leave A Reply