The House of Favourite Newspapers

Dada wa Diamond afanyiwa Kitu Mbaya

0

darleen (7)
Musa Mateja

Kha! Dada wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’, amefanyiwa kitu mbaya na baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki baada ya kumwagiwa maji, pombe, soda na mchanga huku wengine wakimpaka matope mwilini.

darleen (6)Tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri usiku wa kuamkia Novemba 4, mwaka huu kwenye Studio za Wasafi Classic Baby (WCB) zilizopo Sinza-Mapambano, Dar ambapo mrembo huyo alikuwa akitimiza miaka kadhaa tangu azaliwe.

darleen (5)Bila kujua kilichoendelea, Queen Darleen aliitwa mahali hapo usiku mnene na alipofika ndipo akakutana na kitimtim hicho ambacho kwake ilikuwa sapraizi.Habari zilieleza kwamba, ishu hiyo iliandaliwa na Diamond ambaye aliwatonya rafiki zake Queen Darleen kuwa usiku huo angemfanyia sapraizi dada yake huyo lakini hakutaka afahamu hivyo jukumu la kualika watu alimkabidhi rafiki wa mrembo huyo aitwaye Mwengi.

Ilielezwa kwamba baada ya kila kitu kukamilika na muda kutimia, Mwengi alimdanganya Queen Darleen kuwa kuna kitu anataka wakachukue kwenye ofisi hiyo ambapo mrembo huyo alikubali.

darleen (4)Baada ya kutimba mahali hapo, Queen Darleen alikutana na umati, alipoanza kusalimiana nao ndipo wakamzingira na kuanza kummwagia maji, pombe, soda, mchanga na kumpaka matope.
Kufuatia hali hiyo, Queen Darleen alijikuta akiangua kilio kama mtoto

huku akiwaomba wamsamehe kwani alikuwa anaumwa lakini ombi lake halikuzingatiwa kwani waliendelea ‘kumsulubu’ kiasi cha kuishiwa nguvu na kujikuta akilala chini akiwa hoi.
Hata hivyo, walipoona anaweza kupata mshtuko au kuzimia, walimuacha na kuanza kumuimbia ‘happy birthday to you’, jambo lililomshtua na kuanza kumlaumu Mwengi kwa kutomjulisha mapema kwani angeweza kupoteza maisha kutokana na mshtuko alioupata.

darleen (3)Hata hivyo, Meneja wa Diamond, Babu Tale aliwaamuru wamuache na kumshika mkono kisha kumuongoza mahali kulikokuwa kumeegeshwa gari aina ya Toyota Ractis ambalo Diamond alimzawadia kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa.

darleen (2)Baada ya kuoneshwa mkoko huo, Queen Darleen alianza kuangua kilio tena huku akilipiga gari hilo vibao kisha kushukuru kwa kuwa amekuwa akiwaza kuwa na gari kwa muda mrefu.
Akizungumzia tukio hilo, Queen Darleen ambaye ni msanii wa Bongo Fleva aliliambia gazeti hili kuwa katika maisha yake hakuwahi kufanyiwa sapraizi kubwa kama hiyo wala kumwagiwa maji kiasi kile hivyo aliwashukuru wote waliokumbuka siku yake hiyo muhimu.

darleen (1)“Namshukuru sana Diamond kwa kunipatia gari, ni kilio changu cha muda mrefu lakini walichonifanyia ni kitu kibaya kwani wangeniua,” alisema Queen Darleen.Kwa upande wa Diamond aliwashukuru watu kwa kujumuika naye kwenye tukio hilo huku akisema kuwa gari hilo limemgharimu Sh. Milioni 10.

Leave A Reply