The House of Favourite Newspapers

Dakika 360 za Mbelgiji Simba Zinatisha

0

KOCHA mpya wa Simba, Mbelgiji, Sven Vanderbroeck, ameanza vizuri katika timu hiyo baada ya kutimiza dakika 360 sawa na mechi nne akishinda kwa ushindi wa asilimia 100. Mbelgiji huyo aliyechukua mikoba ya Mbelgiji mwenzake, Patrick Aussems, ameiongoza Simba kucheza mechi tatu za Ligi Kuu Bara na moja ya Kombe la FA.

 

Matokeo ya mechi hizo yanatisha na kumfanya kocha huyo kuanza kuwa tisho kwa wapinzani wakiwemo Yanga ambao wanakwenda kukutana nao keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Sven katika mechi ya kwanza tangu aanze kuinoa Simba alicheza dhidi ya Arusha FC, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 6-0 ukiwa ni wa Ligi Kuu Bara.

Mechi za ligi matokeo yake ni; Simba 4-0 Lipuli, KMC 0-2 Simba na Simba 2-0 Ndanda. Mechi zote hizo zimechezwa Uwanja wa Uhuru, Dar.

 

Katika mechi hizo nne, Simba imefunga jumla ya mabao 14, huku ikiwa haijaruhusu bao kitendo ambacho kinawapa matumaini makubwa Simba ya kuibuka na ushindi Jumamosi hii. Cha kufurahisha zaidi ni kwamba, Simba imekuwa hatari zaidi kipindi cha pili katika mechi hizo nne ilizocheza chini ya Sven.

Rekodi zinaonyesha, Simba katika kipindi cha pili kwenye mechi hizo nne tofauti na kipindi cha kwanza. Imeweza kumaliza ikiwa na mabao, huku mara moja pekee ikishindwa kufunga kipindi cha kwanza. Matokeo ya kipindi cha kwanza katika mechi hizo nne ni; Simba 4-0 Arusha FC, Simba 1-0 Lipuli, KMC 0-0 Simba na Simba 1-0 Ndanda.

Leave A Reply