The House of Favourite Newspapers

Kasi ya Sven Yamkimbiza Mbrazil Simba SC

0

RASMI sasa straika mwili jumba wa Simba, Mbrazili Wilker Da Silva Henrique, ameamua kuikwepa mechi ya watani kati ya Simba na Yanga baada ya kuomba kuondoka katika timu hiyo na kukimbilia Malaysia.

 

Wilker ameondoka katika kikosi hicho ikiwa ni siku chache kabla ya Simba kupambana na Yanga katika Kariakoo Derby ambayo itapigwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar. Straika huyo Mbrazili alikuwa mmoja ya Wabrazili watatu ambao walisajiliwa katika dirisha kubwa msimu huu sambamba na Tairone Dos Santos na Gerson Fraga Vieira.

Mtendaji Mkuu wa Simba inayonolewa na Kocha Mbelgiji, Sven Vanderbroeck, Senzo Mazingisa raia wa Afrika Kusini, ameliambia Spoti Xtra, kuwa Wilker alisema: “Wilker ameomba kuondoka katika klabu yetu ikiwa ni baada ya kukaa hapa kwa miezi kadhaa na sisi tumemruhusu, tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya baada ya kukaa hapa.

 

“Tunatambua juu ya mchango wake na tunamshukuru kwa kuwepo hapa kwa muda wote,” alisema Senzo. Mbrazili huyo anaondoka Simba akiwa hajafunga bao lolote katika Ligi Kuu Bara huku akiwa amefunga mabao matatu tu katika mechi za kirafi ki akiwafunga JKT Tanzania, Azam na Orbret TVET.

USAJILI MPYA NI MUDA TU

Katika hatua nyingine Senzo ameongeza kuwa suala la usajili katika klabu hiyo kwa sasa ni suala la muda ambapo wanaendelea na mazungumzo ya mwisho kabla ya kutangaza vifaa vyao vipya. “Kabla hatujasajili tunahusisha wahusika wote kuanzia benchi la ufundi hadi viongozi wa bodi.

 

Tunafanyia kazi sana hilo. Tunategemea kabla ya wiki kumalizika tutatangaza mchezaji mpya ikiwa ni baada ya kumalizana naye kwa kila kitu.

 

“Hatutaki kutangaza mchezaji wakati tukiwa hatujamalizana naye. Lakini pia suala hilo linakuwa gumu kwa sababu hatutaki kuona mchezaji anakuja kutudai baada ya kumsajili ndiyo maana tunachukua muda mrefu katika suala hilo,” alimaliza Senzo.

Leave A Reply