The House of Favourite Newspapers

Dar Live Wanafunga Mwaka Kibabe

0

KWA miaka zaidi ya saba sasa Ukumbi wa Dar Live umekuwa ukifanya makubwa kwenye sikukuu za kufungia mwaka na awamu hii pia hawataiacha Bongo Dar es Salaam salama, hiyo ni kwa kuwa wanatarajia kudondosha shoo ya nguvu katika kuuaga mwaka 2020 na kuukaribisha 2021.

 

Shoo kali ikiwa imesheheni nyota kibao wa muziki wa Bongo Fleva na Singeli watakiwasha kwenye Tamasha la Funga Mwaka na Dar Live katika ukumbi huo uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

 

Shoo hiyo imepewa nguvu kubwa na DJ Tass akishirikiana na madj wengine huku burudani kibao zikimwagika, hiyo ni leo Ijumaa katika siku ya Sikukuu ya Krismasi kwa kiingilio cha elfu tano tu.‘

 

Sapraizi’ kama zote za ma-dj kutoka vituo mbalimbali vya redio, zitakuwepo na tayari wasanii ambao wamethibitisha kulivamia jukwaa la ukumbi huo ambalo ni la kupanda na kushuka ni; Becka Title, Becka Flavor, Pah One, Bonge la Nyau, Suma Mnazareti, Jyga na Wakazi huku mastaa kibao wa Singeli wakithibitisha uwepo wao.

 

Shoo itaanza saa 2:00 usiku hadi majogoo, huku michezo ya watoto pamoja na Disko Toto likirindima kuanzia saa nne asubuhi leo hii.

Stori na Issa Liponda, Dar es Salaam

Leave A Reply