The House of Favourite Newspapers

Dora: Kujiamini Kumenusuru Kifo Changu

0

UKITAJA jina Dora, sio jina geni masikioni mwa mashabiki wa filamu za Kibongo kwa sababu amekuwa ni kivutio kikubwa kwa jinsi anavyoweza kucheza uhusika wake vizuri. Haijalishi jinsi alivyo kutokana na ufupi wake kwani ndio kwanza amezidi kujiongezea mashabiki ndani ya nchi na nje ya nchi.

 

Msanii huyu ambaye jina lake halisi ni Wansekula Zacharia, anasema kujiamini kwake kumemweza kurefusha uhai wake mpaka sasa.

Anasema kama angekuwa mnyonge siku zote basi angeweza kupoteza uhai wake muda mrefu sana. Ungana na AMANI katika mahojiano na msanii huyu kama ifuatavyo hapa chini:

 

Amani: Vipi mambo Dora, upo?

Dora: Nipo dada yangu sina hata pa kwenda kabisa nawaza tu nitoke vipi.

Amani: Kwani si bado uko kwenye tamthilia mbalimbali?

Dora: Ndio lakini za bosi wangu, mlezi wangu Lamata.

 

Amani: Kwani kwanza Dora unaishi pekee yako mpaka Sasa? Nikimaanisha unajitegemea mwenyewe?

Dora: Ndio, mbona muda mrefu sana maana mimi sijakaa na wazazi muda mrefu sana tangu nikiwa mdogo maana nilisoma shule za masista, wakanisomesha mpaka mwisho hivyo kwa wazazi kusalimia tu.

 

Amani: Kwa hiyo ulikuwa ukiishi maisha ya shule tu.

Dora: Nilipomaliza kusoma shule niliendelea kuishi kwenye kituo cha kulelea watoto wanaoishi mazingira magumu, kwa sababu mimi nilikuwa na matatizo ya Seli nundu hivyo ningekaa kijijini ingekuwa ni shida sana hivyo nilisaidiwa nikawa naishi kwenye hicho kituo.

 

Amani: Lakini nyumbani kwa wazazi unaendega kuwasalimia?

Dora: Ndio maana wanaishi Singida.

Amani: Kutokana na kazi yako ya kucheza filamu mbalimbali, unaweza kuwahudumia wazazi wako?

 

Dora: Kabisa bila shaka na wanajivunia mimi kila kukicha na wananishukuru sana kwa vile sikujirudisha nyuma au kuangalia hali yangu na kujiweka kinyonge.

Amani: Kwa nini umesema hivyo.

Dora: Unajua kama mimi nilivyo ningeweza hata kujikatia tamaa au kujiona wa nini lakini ukweli ni kwamba, kujiamini kumeweza kunifanya nifike mbali sana sijui nisemaje maana ingekuwa sijiamini ningeshapoteza maisha muda mrefu mno.

 

Amani: Kwa nini unasema ungekufa?

Dora: Ndio, maana ningezidi kuumwa kwa mawazo lakini huwezi amini mpaka sasa hivi sijisikii chochote labda magonjwa ya kawaida tu.

Amani: Kwenye familia yenu kuna mtu ambaye amezaliwa kama wewe hivyo ulivyo?

Dora: Hapana ni mimi tu lakini najiona bomba kuliko wote sasa (kicheko).

 

Amani: Vipi kuhusu, mahusiano yako, maana ulishasema una mtu wako, bado unaye?

Dora: Ndio aende wapi? Yupo, katulia maana si anajua sipendi ujinga hata siku moja, nikikuambia najiamini unielewe hivyo.

 

Amani: Ulishampeleka nyumbani kumtambulisha?

Dora: Japokuwa yeye anataka lakini kwa upande wangu naona kama mapema mno, asubiri kidogo.

Amani: Nakuonaga siku hizi mara nyingi uko na Kajala, kuna wakati zinaonekana picha kama mmelala pamoja, vipi?

 

Dora: Kajala ni kama ndugu yangu yaani mtu ambaye ananithamini sana, na ninamuita mama, ananipenda sana.

Amani: Kuna kipindi nilikuwa nakuona na Tausi, mnafanya filamu mbalimbali siku hizi sio sana, imekuwaje?

Dora: Ni kwa sababu hatujapata bado filamu za kucheza pamoja maana tukiwa wote kwenye filamu, inakuwa stori hiyo inataka hivyo.

 

Amani: Dora ni msichana ambaye unajipenda sana na unabadilisha mitindo mbalimbali ya nywele, nini siri yako?

Dora: Kwa kweli mimi najipenda sana kwa kila kitu na siri kubwa ni kwamba najiona mwanamke ambaye nahitaji kupendeza kila wakati.

Amani: Haya asante sana Dora.

Dora: Shukrani.

 

MAKALA: IMELDA MTEMA

Leave A Reply