The House of Favourite Newspapers

Darasa: Naheshimu maneno ya linah lakini nina mpenzi!

0

darasaglobaltvonline2Sharif Thabiti Ramadhani ‘Darasa’

Stori: Hamida Hassan, Wikienda

DAR ES SALAAM: Mkali wa Hip Hop Bongo, Sharif Thabiti Ramadhani ‘Darasa’ amefunguka kuwa anaheshimu maneno ya msanii mwenzake, Estalina Sanga ‘Linah’ kuwa anamkubali na kutamani kuwa na mwanaume mwenye sifa kama zake lakini yeye ana mpenzi wake wa muda mrefu.

linahEstalina Sanga ‘Linah’

Akizungumza na Wikienda alipotembelea Global TV Online wikiendi iliyopita, Darasa alisema kuwa Linah ametumia ujasiri kutoa hisia zake na amefurahi kusikia anamkubali ingawa yeye ana mpenzi wake wa muda mrefu na wanaaminiana.

“Namshukuru kwa kunikubali, kiukweli namheshimu na nimefurahi,” alisema Darasa.

Darasa alifunguka hayo baada ya hivi karibuni Linah kueleza hisia zake kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatamani awe na mwanaume mwenye sifa alizonazo Darasa.

Leave A Reply