The House of Favourite Newspapers

‘Dasani Marathon’ Kufanyika Dar Mei 14

0
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola, Nalaka Hetterachchi(kulia) akizungumza na wanahabari.
Rais wa Chama cha Riadha cha Dar Running Club, Goodluck Elvis, akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea
Baadhi ya waandaaji wa mashindano hayo wakiwa katika picha.

MASHINDANO ya riadha ya Dasani Marathon yameandaliwa na kampuni ya Coca-Cola ya jijini Dar es Salaam, yanatarajiwa kuanza Mei 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa mwanariadha mstaafu wa kimataifa, Juma Ikangaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola, Nalaka Hetterachchi, amesema dhamira ya mashindano hayo ni kuendeleza mchezo wa riadha na kukuza uchumi nchini.

Alieleza kuwa sababu ya Coca-Cola kudhamini mbio hizo ni kuonyesha ushirikiano na katika pande zote zinazohusika ili kuinua uzalishaji mali na kuinua michezo.

Washiriki watakimbia katika mbio za kilomita 10 na 21 zikishirikisha zaidi ya wanariadha 1, 000 ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi, na kwamba mshindi wa kwanza atajinyakulia medali.

Kwa upande wake, mwanariadha mstaafu wa kimataifa, Juma Ikangaa, amesema ili mtu apate ushindi katika mashindano hayo ni lazima ajiandae vyema na akawaomba wadau mbalimbali kujitokeza ili kushindania medali hiyo.

Naye Rais wa Chama cha Riadha cha Dar Running Club, Goodluck Elvis, amesema mbio hizo zilizoanzishwa miaka mitatu iliyopita zimekuwa zikipata umaarufu ambapo wamejiandaa vya kutosha ili kuhakikisha usalama unapatikana.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki katika mashindano hayo ambapo alivitaja vituo vya kuchukulia fomu za kujisajili kuwa ni: Colosseum Gym Masaki, Shoppers Supermarket Mikocheni na Mlimani City Mall.

Gharama ya usajili ni Sh. 30,000 katika vituo vyote hivyo ambapo zinaweza kulipwa taslimu katika vituo hivyo au kwa njia ya M-Pesa 243388.

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Leave A Reply