The House of Favourite Newspapers

David Kafulila; ‘Jenerali’ Wa Siasa, Kakulia Chadema, Kang’ara NCCR, Kaula Kwa Rais Samia…Video

0
David Kafulila aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Rais Samia Suluhu Hassan aliwateuwa viongozi sita kuwa Wakuu wa Taasisi mbalimbali akiwemo, David Kafulila aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Kafulila ameteuliwa kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), ikiwa ni miezi 6 tangu Julai 28, 2022 alipoachwa katika uteuzi wa Wakuu wa Mikoa.

Mbali wadhifa wa Mkuu wa Mkoa, Kafulila amewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR-Mageuzi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe na amewahi kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM, lakini kura za maoni hazikutosha.

Safari ya Kafulila ambaye vijana wanamuita ‘Jenerali’ wa siasa za kizazi kipya imekuwa ya kupanda kisha kushuka na sasa amepanda tena na kuibu mjadala kwenye mitandao ya kijamii.

Je, Kafulila ni nani hasa? Global TV inakuletea makala iliyoshiba kuhusu mtu huyu ambaye vijana wengi wanamtazama kama role model wao; David Zacharia Kafulila amezaliwa Februari 15, 1982 mkoani Kigoma; mkoa unaopatikana Magharibi mwa Tanzania.

Kafulila alipata elimu ya msingi katika Shule ya Uvinza kabla ya kuhamia Shule ya Msingi Kinganamo alipomalizia elimu hiyo.

Alisoma elimu ya Sekondari katika Shule ya Wazazi Chumvi kabla kujiunga Shule ya Sekondari ya Shinyanga. ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply