The House of Favourite Newspapers

Mwanamke wa Australia Aliyeshtakiwa kwa Ugaidi Aachiliwa kwa Dhamana

0

 

Waziri wa mambo ya ndani wa Australia Peter Dutton akihutubia kongamano na kupambana na ugaidi mjini Sydney, March 17, 2018.

Mwanamke wa Australia ambaye ameshitakiwa kwa kuingia kwa hiari kwenye eneo linalodhibitiwa na kundi la Islamic State nchini Syria Ijumaa ameachiliwa kwa dhamana na mahakama ya Australia.

Hali limejiri wakati kukiwa na mjadala mkubwa wa iwapo ana hatari yoyote ya kiusalama katika jamii. Mariam Raad mwenye umri wa miaka 31 ni baadhi ya wanawake kadhaa ambao waume zao waliuwawa au kufungwa jela baada ya kujiunga na Islamic State.

Polisi wanasema kwamba Mariam Raad 2014 aliamua kusafiri hadi mashariki ya kati ili kuungana na mumewe licha ya kufahamu kwamba alikuwa akijihusisha na shughuli za kigaidi. Raad alirejeshwa Australia akiwa na watoto wake Oktoba mwaka jana kutoka kwenye kambi ya wafungwa ya inayomilikiwa na wa Kurdi nchini Syria, ili kufunguliwa mashitaka.

Hatua hiyo ni kufuatia uchunguzi uliofanywa na polisi wa New South Wales pamoja na wale wa serikali kuu ya Australia. Raad amefikishwa kwenye mahakama ya mji wa Griffith ilioko takriban kilomita 600 magharibi mwa Sydney, wakati ikiaminika kwamba mume wake aliaga dunia 2018.

Leave A Reply