Davina aanika ‘mazagazaga’…

Davina_1.jpgStaa wa filamu Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’.

Imelda mtema
Staa wa filamu Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’ hivi karibuni alianika ‘mazagazaga’ yake aliyoyapamba kwenye kiuno chake alipokuwa kwenye kibao kata cha ndugu yake kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Future Resort, uliopo Mbezi Beach jijini Dar.

Davina ambaye alionekana mwenye furaha siku hiyo alivalia dera lake ambalo kwa nyuma alilipasua na kuacha sehemu kubwa ya mgongo wake wazi akiwa amejichora ‘tatuu’ huku cheni ya dhahabu ikiwa inaonekana.

“Duuh umemuona Davina hapo mgongoni kajichora vizuri na akigeuka kwa mbele huwezi kujua kabisa kama nyuma yupo wazi lakini kwa upande wangu mimi naona kapendeza sana,” alisikika mtu mmoja ambaye alihudhuria katika sherehe hiyo.


Loading...

Toa comment