The House of Favourite Newspapers

DC JERRY MURO APAMBANA NA WATIA MIMBA MADENTI – VIDEO

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akizungumza.

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro kwa kushirikiana na Jeshi la polisi Wilaya ya Arumeru limewakamata watuhumiwa watatu ambao wameshiriki kumtoa mimba mwanafunzi wa kidato cha nne kwa kutumia dawa za miti shamba suala ambalo linachochea mimba kwa wanafunzi na kuzorotesha elimu yao.

 

 

Akizugumzia tukio hilo Dc Jerry Muro amesema kuwa wamebaini tukio hilo baada ya kuweka mtego na kuwabaini watuhumiwa hao pamoja na watia mimba ambao wamefikishwa polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.

 

 

Akielezea jinsi alivyopewa ujauzito na kisha ujauzito kutolewa mmojawa wadaiwa kupewa ujauzito (jina limehifadhiwa)  amesema ni kweli alipata ujauzito kwa kurubuniwa na kijana wanaeishi naye jirani nyumbani ambaye alikuwa akimrubuni kwa kumpatia fedha.

 

 

Kwa upande wao watuhumiwa wa sakata hilo kijana aliyedaiwa kumpa mimba binti, pamoja na mama mzazi wa (mwanafunzi mtendewa) na mwanamke ambaye ni ndugu wa kijana aliyempa mimba ambaye anatajwa kuhusika na kumtoa ujauzito  wametoa sababu mbalimbali ambazo hata hivyo zimeonekana kukinzana zenyewe  kutokana na mama wa binti kukiri kuwafahamu watuhumiwa wenzake na kuelezea tukio la mchezo mzima ulivyokuwa.

 

 

Kutokana na tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amevigiza vyombo vya Usalama kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote ambao wamehusika katika tukio hilo , ambapo pia amelitaka jeshi la Polisi kuhakikisha wanawakamata na wanawafikisha mahakamani watu wote waliohusika katika kuwapa ujauzito wanafunzi 57 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

 

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

 

Comments are closed.