The House of Favourite Newspapers

DC Kibaha, Mbunge Koka Wameongoza Harambee Uzinduzi Wa Filamu

0

MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Assumpta Mshama na Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka, jana wameongoza harambee ya kuuza DVD ya muigizaji Luckiness Mokiwa iitwayo Kashinde.

Tukio hilo lilichukua nafasi kati Ukumbi wa River Road, Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani ambapo awali, ulifanyika uzinduzi wa DVD hiyo kisha mkuu huyo wa wilaya kuongoza harambee ya uuzwaji wake.


Mbunge Koka alichangia kiasi cha shilingi milioni moja huku DC huyo akichangia shilingi milioni 5 na viongozi wengine wa Serikali wakiwemo madiwani na wenyeviti wa mitaa wakiinunua DVD hiyo kwa viwango tofauti.

Kwenye hafla hiyo, msanii wa Bongo Fleva, Snura Mushi, alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza jukwaani.
Mwishoni, muigizaji Luckiness Mokiwa, aliwashukuru watu wote waliojumuika kwenye uzinduzi na uuzwaji wa DVD hiyo na kuwaomba wanunue nakala orijino kwani itaanza kusambazwa na Kampuni ya Steps Entertainment kuanzia Jumatatu (kesho) ijayo.


“Nawashukuru sana Steps kwa kuanza na kazi yangu maana walikuwa wamesimama kidogo kusambaza lakini wamerudi na kuanza na mimi,” alisema Luckiness.
Pia alimshukuru mkuu wa wilaya, mbunge na mumewe ambaye alichangia shilingi milioni 2 kwa kununua kazi yake hiyo.

Aidha, Luckiness alitumia nafasi hiyo pia kutoa tuzo mbalimbali za heshima kwa watu ambao wametoa mchango mkubwa sana katika sanaa yake wakiwemo wazazi wake mzazi, Mr & Mrs Vicent Mokiwa.

Na Erick Evarist

Leave A Reply