DENTI ATEKWA KIMAFIA, BABA YAKE ASIMULIA – VIDEO

 

HUU ni zaidi ya umafia! Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja jijini Dar, mwenye umri wa miaka 16 (jina tunalihifadhi kwa sababu za kimaadili) ametekwa asubuhi na mapema alipokuwa njiani kuelekea shuleni.  Tukio hilo la kikatili lilitokea Julai 8, mwaka huu maeneo ya Karume wakati aliposhuka ili kubadili basi lingine. Akizungumza na Risasi Jumamosi, mwanafunzi huyo alisema kuwa siku hiyo alitoka nyumbani asubuhi sana kuelekea shuleni.

 

“Nilipanda daladala kuelekea Karume, nilipofika pale nilishuka kwa kuwa nilikuwa naenda Mnazi Mmoja, nikawa natakiwa nipande gari jingine nikapata wazo la kuingia sokoni Karume niangalie viatu.

 

“Kabla sijaingia ilikuja gari aina ya Toyota IST nyeupe ikasimama, dereva akaniita jina langu (analitaja), nikawa sijamfuatilia akaita tena kwa mara nyingine nikajua atakuwa ananijua acha nikamsikilize.

“Nikaenda akaniambia yeye ni rafiki wa baba yangu; nikamuuliza huyo anayesema baba yangu anaishi wapi? Akanijibu anaishi Kinondoni. “Kwa kuwa baba yangu ni maarufu nikajua ni kweli wanafahamiana.

AMUINGIZA KINGI

“Akaniuliza naenda wapi? Nikamwambia naelekea shule lakini kwa kuwa muda bado naingia kuangalia viatu vya shule. “Akaniambia nitakuja kuangalia siku nyingine nipande gari anipeleke shuleni, kwa kuwa aliniambia anamjua baba yangu sikuwa na mashaka naye nikapanda tukaenda mpaka mataa ya Kariakoo, akageuza. Nikamwambia hii njia mbona

siielewi? Akasema nimsikilize yeye tukaelekea barabara ambayo tulikuja kutokea Amana pale ndio napakumbuka, tukaingia uchochoroni hivi tukashuka tukaelekea kwenye nyumba moja ipo ndanindani, akanipeleka kwenye chumba kimoja nahisi ndipo kwake, nikapatambua ni Buguruni. Akaondoka huku akinitisha kuwa nikipiga kelele nitakiona cha mtema kuni na kuniacha pale akarudi siku ya Jumanne asubuhi.

AMLETEA SUPU

“Alirudi akiwa na supu akaniambia ninywe; mimi nikakataa mlango aliufunga na funguo na mimi hata ile akili ya kupiga kelele nikawa sina, mawazo yangu yalikuwa nyumbani kwa kuwa sijawahi kulala nje na nyumbani.

“Akatoka tena akarudia kunitisha na kunionya nisipige kelele, alirudi mida ya saa moja usiku, akaanza kunigombeza na kuniambia kwa nini sitaki kula na nipo chini yake nikiendelea mfanyakazi, mfanyabiashara, mwekezaji na mjasiriamali mwenye kipato pengine kuliko hata baadhi ya wanaume. “Sasa mwanaume aliyeoa mwanamke mwenye kazi, anayejiamini katika maisha akifanya jambo hata la bahati mbaya huonekana ana kiburi na hivyo kuchukiwa na mwanaume kwamba hamtii,” alisema.

TOFAUTI YA HISIA NALO NI TATIZO

Kwa mujibu wa Marcus Buckingham, mhamasishaji na mshauri wa masuala ya kibiashara nchini Uingereza amewahi kusema kuwa kinachowatofautisha wanawake na wanaume kwenye suala la kuumizwa kimapenzi ni hisia  “Nikamkubalia ila yule mama alikawia sana kurudi, na aliporudi nikamwona baba yangu, akaniambia wananitafuta tangu Jumatatu kumbe yule mama alikwenda kupiga simu baada ya kuniona ndio ndugu zangu wakafika eneo hilo.

“Baada ya hapo baba akatuchukua wote pamoja na wale watoto, akatupeleka kituo cha Polisi Oysterbay, baba akapewa namba za simu za yule dada na mtoto wake mkubwa tuliyekuwa naye, akampigia huyo dada kuwa watoto wake wapo kituoni hawatatoka mpaka Jumatatu aje.

“Kweli yule dada alimpa taarifa kaka yake (aliyemteka mwanafunzi huyo) wakaja pamoja pale kituoni ndipo wakakamatwa.” Naye baba mzazi wa mtoto huyo, Hajji Said alisema:

“Mwanangu aliondoka nyumbani kuelekea shuleni lakini ilipofika usiku nilipoona hajarudi ikabidi niende kutoa taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Mwananyamala, nikaambiwa mpaka saa 24 zipite niende Kituo cha Polisi Oysterbay.

“Kweli yalipopita nikaenda Oysterbay nikafungua jalada la taarifa lililosomeka OB/ RB/5961/2019 TAARIFA, na kuambiwa kuwa tushirikiane kumtafuta ndipo nilipoamua kumposti picha yake mtandaoni.

“Hatimaye siku ya Jumapili nikapigiwa simu na mama mmoja kuwa mwanangu ameonekana Sea Cliff Hotel nikapanda pikipiki haraka nilipofika hotelini hapo nikamkuta mwanangu akiwa na watoto wengine watatu, nikawapigia ndugu zangu simu wakanishauri nimuulize kilichomsibu.

“Nikawachukua nikawapeleka Polisi Oysterbay, tukampigia simu huyo dada mwenye watoto wake ambapo alisema yeye alikuwa hajui kama mtoto huyo ametekwa kwa kuwa kaka yake aitwaye Juma ndiye alimletea kwake na kuomba kukaa naye kwani amemuokota na wazazi wake wamefariki dunia. “Na mimi nikamwambia siwaachii watoto wake mpaka huyo Juma afike na kweli alifika wote wakawekwa ndani,” alimalizia.

Shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Temba, aliwatahadharisha wazazi kuwa makini na kuwafundisha watoto mitego mbalimbali ya watekaji. Alipotafutwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Mussa Taibu na kuulizwa kuhusu tukio hilo alisema halijamfikia. “Hilo suala halijafika mezani kwangu lakini nitafuatilia,” alisema.

Msichana ALIYETOWEKA, Apatikana HOTELI ya KITALII..


Loading...

Toa comment