The House of Favourite Newspapers

DHAHABU NA MAMILIONI YA FEDHA VYAKAMATWA MWANZA (PICHA +VIDEO)

Gari aina ya Toyota Land Cruiser Kruger likiwa na begi lenye fedha taslimu zaidi ya Tsh. Milioni 360

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limekamata kilo 323.6 za Dhahabu na fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni mia tatu na Milioni tano (305,000,000) jana  zikisafirishwa kuelekea mkoani Geita, ambapo watu watatu wanashikiliwa mpaka sasa kwa kosa la kusafirisha Dhahabu hizo kinyume na utaratibu.

Akizungumza baada ya kushuhudia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewaonya Askari wasaliti au yeyote yule aliyeshiriki katika matukio hayo kwani ni sawa na msaliti wa nchi na kutoa maagizo kwa Jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha wahusika wote wanapatikana.

Dhahabu zilizokamatwa.

 

Comments are closed.