The House of Favourite Newspapers

Diamond Amkuwadia Wolper kwa Harmonize

0

Diamond-PlatnumzDiamond Platnumz

DAR ES SALAAM: Ama kweli penzi ni kikohozi, kulificha huwezi. Baada ya usiri mzito kutawala, hatimaye imebainika kuwa The Big Boss wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ndiye ‘aliyeinjinia’ penzi jipya mjini la muigizaji Jacqueline Wolper na kijana anayekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’.

3-7-390x210Harmonize na Wolper

RISASI LILIANZA KUTONYWA

Awali, gazeti hili lilitonywa kuhusu penzi hilo jipya na chanzo chake makini na kueleza namna ambavyo Diamond alivyokuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha Hamonize ambaye ni memba wa WCB ‘anamng’oa’ Wolper.

“Diamond ndiye aliyesimamia mchakato mzima. Katumia kila mbinu kuhakikisha Wolper anaingia kwenye himaya ya mdogo wake. Nafikiri pia atakuwa ameangalia na suala zima la kibiashara, muziki sasa hivi unataka msanii azungumzwe,” kilisema chanzo hicho.

harmonize kasuku - bekaboyHamonize

DOGO NDIYE ALIANZA KUSUMBUA

“Hamonize ndiye aliyeanza kuvutiwa na Wolper. Akamwelezea Diamond hisia zake, kama unavyojua tena Diamond si mtu wa kuremba, fasta tu akaweka mambo sawa. Kila kitu kikaenda kwenye mstari,” kilisema chanzo chetu.

WOLPER-2.pngWolper na Mkongo.

MKONGO HANA CHAKE

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kutokana na Diamond kumwaga ‘sumu’ za kutosha na Wolper kuingia penzini ‘mzimamzima’ ndani ya muda mfupi, Mkongo aliyekuwa anammiliki mrembo huyo hana tena chake kwa sasa.

“Aaah! Mkongo hana chake tena kwa sasa. Wolper hasikii wala haoni. Amechanganyikiwa na penzi la Hamonize kiasi ambacho hataki kusikia habari ya mwanaume mwingine yeyote,” kilisema chanzo hicho.

wolperWolper

MAMBO HADHARANI MITANDAONI

Mara baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu huo, wakati Risasi Mchanganyiko likiendelea kufanya uchunguzi wake, ghafla likakumbana na video ya wawili hao kupitia mtandao wa kijamii wa ‘Snap Chat’ ambayo ilimuonesha Wolper akiwa ‘hajiwezi’ kwenye gari akiimbiwa wimbo wa Number One wa Diamond na Hamonize aliyekuwa akiendesha gari hiyo.

****GAZETI LA RISASI JUMATANO LINA KILA KITU KUHUSU UBUYU HUO****

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply