The House of Favourite Newspapers

Diamond Ampongeza Makonda Dar

Nasib Abdul ‘Daimond Platnumz’

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva,  Nasib Abdul ‘Daimond Platnumz’, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda kwa jitihada zake kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa salama.

Mrisho Mpoto na Banana Zoro wakitumbuiza

“Kwanza kabisa Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda kwa jitihada zake. Ukizingatia ni mwaka mmoja tu tokea awe mkuu wa mkoa lakini utendaji wake umezaa matunda mengi na changamoto ni nyingi zinazo mkabili lakini bado amekuwa imara.”, alisema Diamond.

Meneja wa Diamond wa kwanza Kushoto akizungumza jambo na Diamond

Diamond ameyasema hayo leo katika mkutano  kuhusu vita dhidi ya madawa ya kulevya uliofanyika katika Bwalo la Polisi Oster Bay jijini Dar es Salaam ambako Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na viongozi wengine wa serikali na taasisi mbalimbali walihudhuria.

Waathirika wa madawa ya kulevya na wadau wengine walihudhuria mkutano huo
Viongozi wa Dini nao walihudhuria mkutano huo
Meza kuu ilivyoonekana

Comments are closed.