The House of Favourite Newspapers

Diamond Platnumz Afunguka Tetesi za Kumtenga Dyllan Aliyezaa Hamisa Mobeto

0

Diamond Platnumz; ni msanii mkubwa wa muziki wa Kizazi Kipya.

Diamond Platnumz; ni msanii mkubwa wa muziki wa Kizazi Kipya ambaye kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya tetesi za mitandaoni kwamba anamtenga mtoto Dyllan aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Diamond amesema kuwa, anaumizwa namna ambavyo mama wa mtoto anamuweka mwanawe huyo kwani huko ni kumuumiza mtoto ilihali mtoto ni malaika na hajui kitu.

Amesema kuwa, mama wa mtoto (Hamisa) ndiye anayejua baba halisi wa mtoto kwani hata yeye (Diamond) alikuja kumjua baba yake akiwa tayari ni mkubwa hivyo asingependa jambo kama hilo kwa mtoto huyo.

Diamond amesema kuwa, amekuwa akisaidia watu wengi na watoto hivyo hajali suala la mtoto ni wa nani badala yake anamsaidia kama anavyowahudumia watu wengine ambao siyo hata ndugu zake.

Leave A Reply