The House of Favourite Newspapers

Diamond Platnumz Ashinda Tuzo za MTV EMA Kipengele Cha Best African Act.

0

Msanii wa Diamond Platnumz usiku wa kuamkia leo amewatoa kimasomaso Watanzania baada ya kuibuka mshindi katika Tuzo za MTV EMA katika kipengele cha Best African Act.

Katika kipengele hicho, Diamond alishindanishwa na wasanii wakubwa wakiwemo Burna Boy na Asake wa Nigeria, Libianca kutoka Cameroon na Tyler ICU kutoka nchini Afrika Kusini.

Ushindi wa Diamond katikati ya msitu wa wasanii hao wakubwa, ni jambo ambalo halikutarajiwa na wengi na ndiyo maana baada ya orodha ya washindi kutoka, gumzo limekuwa kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wengi wameoneshwa kufurahishwa na Diamond hasa kwa kuwaangusha miamba ya Nigeria, Asake na Burna Boy na kuwataka wasanii wengine kuiga mfano huo.

Kwa upande wa Wanaigeria, ushindi wa Diamond haujawafurahisha baadhi ya Wanigeria kuanza zengwe mitandaoni kwamba kulikuwa na figisu, jambo ambalo wenyewe kwa wenyewe walianza kupingana.

Leave A Reply