The House of Favourite Newspapers

Diamond Platnumz Kolabo Na Rapa Tyga ni Milioni 300.7 (VIDEO)

 

MSANIIwa Tanzania, Naseeb Abdul Juma,  maarufu kama Diamond Platnumz, amefunguka juu ya gharama za kufanya kazi na rapa mkubwa wa Marekani wa lebo ya Young Money, Micheal Ray Stevenson,  maarufu kama ‘Tyga’.

 

Akizungumza kwenye mkutano baina ya wasanii na Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) ambao ulihusu suala la asilimia ya malipo kwenye nyimbo za wasanii, Diamond alisema alitaka kufanya kolabo na mwanamuziki  Tyga ambaye alitaka  Dola 150,000 (Tsh.Milioni 300.7).

 

 

Rapa Tyga anatoka katika lebo kubwa nchini Marekani inayomilikiwa na Lil Wayne, ‘Young Money’.

Lebo nyingine ni Last Kings Records, Def Jam Records, Republic Records, Empire Distribution, Cash Money, Universal Motown Records, Decaydance na Good Music.

 

Tyga ni rafiki mkubwa wa msanii Chris Brown ambapo wakati huu anafanya vizuri na nyimbo zake mbili za mwaka huu za ‘Girls have fun’ na ‘Floss in the bank’.

 

TAZAMA VIDEO ALICHOKISEMA

 

 

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.