The House of Favourite Newspapers

Diarra Ampa Mbinu Mshery Yanga

0

BAADA ya kutua Yanga, kipa Aboutwaleeb Mshery, amefunguka kuwa ana matumaini makubwa ya
kupata nafasi katika kikosi cha
kocha Nabi kwani amekuwa akijifunza vitu vingi kutoka kwa kipa namba moja wa timu hiyo, Djigui Diarra kwa kipindi chote ambacho alikuwa na Mtibwa.


Amesema anaamini katika
kujifunza kwa makipa wenye uwezo mkubwa na kuongeza bidii zaidi ili kumshawishi mwalimu.

 

Yanga ilimtambulisha rasmi mchezaji huyo jana (juzi) kama kipa wao. Akizungumza na Championi Ijumaa, Mshery alithibitisha kuwa mipango yake baada ya kujiunga na familia ya Wanajangwani ni kuhakikisha anapambana ili aweze kumshawishi Nabi aweze kumpa nafasi ya kuanza lakini pia amekuwa akijifunza vitu vingi kutoka kwa makipa wakubwa kama Diarra ambaye atakwenda kuchezaAfcon akiwa na kikosi cha Mali.


“Kwanza kabisa nina
furaha ya kujiunga timu kubwa kama Yanga lakini nina kazi kubwa ya kuhakikisha napambana ili niweze kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kocha Nabi.


“Diarra ni kipa mzuri na
nimekuwa nikimfuatilia kwa kipindi kirefu, pia nimejifunza vitu vingi sana kupitia yeye,
hivyo kucheza naye timu
moja kwangu ni jambo zuri na ninaamini nitajifunza vitu vingi kupitia yeye lakini pia kikubwa nahitaji zaidi ushirikiano kutoka kwa makipa wenzangu Erick Johora na Djigui Diarra, pamoja na wachezaji wenzangu ili tufikie malengo ya Yanga ambayo ni kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema Mshery.

STORI: HAWA ABOUBAKHARI NA HUSSEIN MSOLEKA

 

 

Leave A Reply