The House of Favourite Newspapers

Diarra, Aucho Wanogesha Kambi ya Yanga Morocco

0

JUMLA ya wachezaji wanne wa Yanga, leo Jumanne wanatarajiwa kujiunga kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Morocco tayari kwa kuanza maandalizi ya msimu mpya.Kikosi hicho juzi Jumapili mchana kilisafiri kuelekea Morocco ambapo kitaweka kambi ya siku kumi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema leo Jumanne wachezaji wanne wanatarajiwa kujiunga na kambi hiyo ambao ni Yannick Bangala Litombo, Djigui Diara, Khalid Aucho na Yacouba Songne ambao hawakuwepo katika msafara wao.

 

Aliongeza kuwa, mara baada ya jana Jumatatu kikosi kufika huko Morocco, leo Jumanne wataanza mazoezi.

 

“Leo (Jumatatu) asubuhi tunatarajiwa kuanza safari ya kuelekea Morocco baada ya kupumzika hapa Dubai.“Kesho (leo Jumanne) wachezaji wanatarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja baada ya wale wachezaji ambao hawakuwepo katika msafara wetu kuripoti kambini.

 

Wachezaji hao ni Diarra, Aucho, Yacouba na Litombo ambaye yeye alikuwepo hapa Morocco akisubiri kuungana na wachezaji wengine wapya,” alisema Mwakalebela.

Leave A Reply