The House of Favourite Newspapers

Dillian Whyte Amnyamazisha Tyson Fury Katika Mtandao wa Kijamii

0
Antony Joshua

BONDIA Tyson Fury ambaye alipambana pambano baina yake na Dillian Whyte mnamo Aprili 23, mwaka huu na kuibuka mshindi katika pambano hilo, Tyson Fury asema katika mtandao wa kijamii kuwa ameahirisha pambano baina yake na Anthony Joshua baada ya mkatataba kuisha mda wake bila kusainiwa kudhihirisha kuwa pambano lake na Anthony Joshua halijapitishwa.

 

Lakini Dillian Whyte anaamini kuwa Fury anajaribu kukwepa pambano lake na Anthony Joshua na kumshauri aache pambano liendelee hapaswi kuwa na haraka sababu mapambano kama hayo huchukua muda mrefu kidogo katika maandalizi yake na pesa nyingi kwahivyo hana budi kusubiri.

Tyson Fury

Dillian Whyte ameendelea kwa kusema kuwa:

“Fury anahitaji atulie na asiwe na papara na kuharakisha jambo kubwa kama hilo”, akaongezea kuwa “moja wapo ya njia ambazo anatumia Fury katika majadiliano ya bishara huwa ni kupiga tu kelele katika mitandao ya kijamii na kuishia kuita watu wasio na makazi (homeless), kwahiyo Tyson Fury inabidi afunge mdomo wake na kuacha pambano liendelee”.

Dillian Whyte

Pambano hilo kwa sasa limesitishwa na hakuna dalili za kuonesha kuendelea kwake kwa sababu Fury ameweka wazi katika video aliyoisambaza katika mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa tarehe ya mwisho imeshafika hapo saa kumi na moja jioni siku ya jumatatu ambapo hakuna makubaliano yaliyofikiwa juu ya pambano hilo.

 

Aidha Anthony Joshua amesema alikuwa anachukua ushauri kwa uongozi wake na alipanga kusaini mkataba huo siku ya jumapili, Hivyo Whyte amwambia Fury kuwa yeye yuko tayari kupambana na Anthony Joshua Disemba mwaka huu endapo ataendelea kujizungusha na kuwa muoga wa kurudisha pambano liendelee.

 

Imeandikwa na Arafat Ramadhan Salem kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply