The House of Favourite Newspapers

Dimbwi la Damu-10

Maisha yao yaliendelea 
vizuri  katika jiji la Ottawa 
nchini Canada! Kwa pesa aliyokuwa nayo Shabir alifungua  vituo vya mafuta kumi na sita katika jiji hilo, vilimchanganyia kiasi cha kutosha na kwa kutumia ujanja wa kukwepa kodi aliotoka nao Tanzania alizidi kujitajirisha kiasi kwamba katika muda wa miaka mitano alikuwa miongoni mwa mamilionea  nchini Canada.

Ilikuwa ni familia yenye furaha na  maisha ya Victoria yalikuwa mazuri kupita kiasi, wakati huo alikuwa   kidato cha tatu katika shule ya  St. George, ilikuwa ni shule maarufu ya vipofu nchini Canada.

Tayari Victoria alikuwa msichana aliyekomaa alishavunja ungo!  Alipelekwa shuleni na gari na alinunuliwa nguo nzuri na mpya karibu kila baada ya miezi mitatu! Ilikuwa si rahisi hata siku moja kugundua hakuwa mtoto wa familia hiyo, kitu pekee kilichowafanya watu wahisi hakuwa mtoto wa Shabir  ni rangi ya ngozi yake.

Shabir na Leah kwa maisha na matunzo waliyompa  Victoria walifikiri  alikuwa na raha sana  katika maisha yake lakini ukweli haukuwa huo, alikuwa ni miongoni mwa watu wenye huzuni sana duniani  na yote hiyo ilikuwa ni sababu ya kaka yake Nicholaus! Kila siku alimkumbuka  na kulia machozi, chakula na mavazi aliyopewa hayakutosha, siku zote aliamini Nicholaus  pekee ndiye alikuwa furaha yake.

******************

Nicholaus alizidi kuning’inia huku akiyagusa maji kwa mikono yake bila kujua ni kitu gani kilikuwa kimeng’ang’ania shati  na suruali yake kwa juu! Ghafla aliona kitu kama kenge mkubwa kikiyakata maji kumfuata, alipoangalia vizuri aligundua ni Mamba! Akajua alikuwa chakula chake siku hiyo, kifo alianza kukiona karibu yake kwa mara nyingine na alitetemeka mwili mzima.

Lakini alishangaa kuona anavutwa kutolewa ndani ya bwawa huku akisikia miungurumo ya wanyama wenye hasira shingoni kwake! Alijikuta akitupwa kwenye nyasi na  wanyama hao walimvamia hapo hapo ardhini na kuanza kumshambulia. Walikuwa ni mbwa wakali na wakubwa kama ndama, aliwakumbuka mbwa hao waliokuwa wakimkimbiza kabla hajadumbukia ndani ya bwawa.

Pamoja na kuumwa sana na mbwa shingoni na matakoni bado Nicholaus alifurahi kwa sababu alikuwa ameokolewa, kwani alijua wazi bila mbwa hao kumnasa na kumtoa ndani ya bwawa ni lazima angeliwa na Mamba na huo ndio ungekuwa mwisho wake! Angekufa bila kumwona dada yake Victoria jambo ambalo hakutaka kabisa litokee na alimwomba Mungu aliepushe.

“Stooooooop!” (Achaaaa!) Ilikuwa ni sauti nzito ya mwanaume ikitokea upande wa pili,  mbwa wote walitii amri hiyo na kuacha kumuuma Nicholaus! Alikuwa ni mwanaume mrefu na mnene na mwenye ndevu nyingi kama ilivyo kawaida ya watu wa Iran.

Alianza kumsemesha  kwa lugha ya Kiirani lakini Nicholaus hakuelewa kitu kilichosemwa, alibaki amekusanya mikono yake miwili na kupiga magoti chini akimwomba msamaha mwanaume huyo aliyeonekana kuwa mlinzi akiwa na gobole lake mkononi.

“Forgive me and please save my life!”(Nisamehe na tafadhali okoa maisha yangu)

“You….! You…! Are you engrish?”(Wewe…! Wewe…! Wewe ni Muingereza?) Aliuliza mlinzi huyo kwa kiingereza kibovu akitaka kujua kama Nicholaus alikuwa Muingereza.

“I’m a Tanzanian!”(Hapana mimi ni Mtanzania!) Alisema Nicholaus na mwanaume huyo alimmulika tochi na kumwangalia kwa makini usoni.

“Ha!My God!”(Ha! Mungu wangu!) Mlinzi alionekana kushangaa alipoiona sura ya Nicholaus na palepale alianza kumvuta kumrudisha hospitali.

****************

Akiwa kidato cha nne katika shule ya sekondari  ya vipofu ya St. George, Victoria alishabadilika kiasi cha kutosha! Alikuwa msichana mrefu mwembamba na zaidi ya sifa hizo  alikuwa na umbile la kike haswa! Alikuwa amebadilika  kutoka   umbile la minyoo  hadi umbile la herufi  ‘d’

Alijaliwa maumbile  makubwa kwa nyuma yaliyotingishika kila alipotembea, alikuwa na mguu mkubwa uliojaza kama chupa ya bia aina ya Primus! Kifupi katika wakati huo Victoria alimvutia kila mtu aliyemwona na haikuwa rahisi kugundua  alikuwa kipofu kama mtu alimkuta amekaa kwa jinsi alivyoonekana mzuri!

Wakati mwingine alipojipapasa kwa nyuma na kujilinganisha na wasichana wenzake aliowagusa waliokuwa na maumbile ya kizungu shuleni aligundua maumbile yake hayakuwa ya kawaida!

“Mama au mimi nina ugonjwa?” Victoria alimuuliza Leah baada ya kugundua umbile  lake halikuwa la kawaida.

“Kwanini?”

“Hili umbile langu linanishangaza, wanafunzi shuleni wananizomea sana!”

“Mbona hata mimi nilikuwa hivyo! Huo si ugonjwa”

Kwa Victoria, Leah alikuwa ni kama mama yake, alihesabu ndiye ndugu peke yake aliyekuwa  amebakiza  duniani,   hakumhesabu tena kama mtumishi wa ndani kama ilivyokuwa  wakati wa uhai wa wazazi wake! Siku zote alimwita Leah mama na Leah alimchukulia Victoria kama mtoto ingawa walipishana miaka michache sana kati yao.

Shabir alimpenda Victoria kuliko hata  Manjit mtoto wake  wa kuzaa! Alimpa Vicky kila alichohitaji katika maisha yake, kila siku za Jumapili ilikuwa ni lazima amshike mkono na kumtembeza sehemu mbalimbali za jiji la Ottawa na alifanya hivyo kwa madai ya kutaka kumfanya ajisikie vizuri!

Kwa upendo huo wa Shabir ulimfanya Victoria alizidi kujisikia kupendwa, kitu pekee kilichopungua maishani mwake kilikuwa ni Nicholaus kaka yake alitamani angekuwepo Canada ili wafaidi maisha pamoja.

“Sijui hivi sasa atakuwa wapi Nicholaus,  nafikiri atakuwa yupo hai mahali fulani, si ajabu siku moja nitapokea simu kutoka kwake nina uhakika siku hiyo ndiyo itakuwa siku ya furaha kuliko zote maishani mwangu!” Aliwaza kila mara Victoria.

*********************

Wakati Shabir anamwoa Leah huko Arusha miaka mingi kabla ya kuhamia Canada, Leah alikuwa kitu cha uhakika, alikuwa mrembo  kupindukia! Maumbile yake  ya nyuma  yalikuwa ya utatanishi, mtoto alijaliwa na akajaliwa kwelikweli!  Ni kitu hicho ndicho kilichomchanganya akili Shabir.

Siku zote alipenda sana wanawake wenye makalio makubwa! Hata mke wake aliyekuwa naye kabla ya kumuoa Leah alikuwa hivyo hivyo, nguo zake alilazimika kupima   kwa mafundi cherehani hakupata nguo za kununua moja kwa moja dukani,  zilimbana kupita kiasi na kuchanika siku chache tu baada ya kuzinunua.

Shabir alipenda maumbile ya namna hiyo! Na hivyo ndivyo alivyokuwa Leah lakini baada ya  kumzaa   Manjit na kumnyonyesha maumbile yake yalianza kusinyaa na mwili wake ulianza kuporomoka! Makalio yake makubwa  yakapotea   na kujikuta  amepigwa randa!

Jambo hilo lilipunguza  sana mapenzi ya Shabir kwa mkewe lakini asingeweza kumwacha kwa sababu hiyo,alizidi kuvumilia sababu walikuwa na mtoto wao mzuri Manjit!

Ingawa hakuna mtu katika familia yake aliyelijua jambo hilo lakini Shabir alikuwa miongoni mwa watu waliovutiwa sana na maumbile na mabadiliko ya Victoria kimwili, alifurahi kila alipomwona Victoria akitembea mapigo ya moyo wake yalienda sambamba na mitetemo ya maungo ya Victoria kila alipotembea.

Tangu wakati huo Shabir alibadilisha hata aina  na mitindo ya nguo  alizomnunulia Victoria akawa ananunua nguo za kumbana na viblauzi vilivyoacha kifua  na sehemu ya matiti ya Victoria wazi! Mke wake alifikiri ni jambo la kawaida lakini lengo la Shabir lilikuwa si jema  alitaka kuyaona maumbile ya Victoria.

Leah  aliendelea kuichukulia hali hiyo kama mapenzi ya baba kwa mtoto, hata siku moja  hakuwahi kuwaza kuwa mumewe angeweza kumtamani Victoria kimapenzi.

Upendo wa Shabir kwa Victoria ulizidi  kuongezeka siku hadi siku hadi alipomaliza kidato cha nne, ingawa  Victoria alikuwa kipofu ilifikia wakati akawa analazimisha kwenda naye kwenda tafrija za wafanyabiashara wenzake usiku akimwacha mke wake nyumbani!

Leah  hakushangazwa na mambo hayo alizidi kuitafsiri hali hiyo kama mapenzi ya kizungu kwa watoto, jambo ambalo watu wengi  nchini Canada walilifanya! Halikuwa jambo la ajabu baba kutembea amemkumbatia mtoto wake wa kike au mama kutembea akiwa amekumbatiwa na mtoto wake wa kiume.

Katika  tafrija alizokwenda na Victoria, Shabir alicheza naye muziki  akiwa amemkumbatia,  wafanyabiashara wenzake walifurahi kuona mzazi akimchangamsha mtoto wake kipofu.

“I’m trying to make my daughter enjoy life! Being blind doesn’t mean staying at home all the times!”(Ninajaribu kumfanya mtoto wangu afaidi maisha kwani kuwa kipofu haimaanishi kukaa nyumbani muda wote!) Shabir aliwajibu watu kila walipoonekana kumwangalia.

“Is she your daughter?”(Huyo ni binti yako?)  Watu wengi walimuuliza.

“Yes, My foster child!”(Ndiyo mtoto wangu wa kufikia)

Ingawa alijua wazi mawazo yake yalikuwa yakimpeleka pembeni, homa ya mapenzi ya Shabir kwa Victoria iliendelea kuongezeka siku hadi siku, kila Victoria alipopita mbele yake alihisi damu mwilini mwake ikisisimka na  pamoja na  upofu wake mara kwa mara  alimtuma vitu.

“Bwanae! Mtoto kipofu huyu akalete maji ya nini wakati sisi  wenye macho tupo?” Leah alisema siku moja Shabir alipomtuma Victoria maji.

“Basi hata wewe  kalete, lakini nilitaka afanye mazoezi kidogo!” Shabir alisema akiwa na amejawa na aibu.

Tabia ya Shabir ilibadilika kupita kiasi  mpaka Leah akaanza kuhisi vibaya  huo! Ugomvi ulianza kujitokeza mara kwa mara ndani ya nyumba yao kisa kikiwa Victoria hasa baada ya Leah kumzuia Shabir kuwa anatoka na Victoria nyakati za usiku.

Pamoja na ugomvi wao kufanyika chumbani bado Victoria aligundua  kuwa yeye ndiye alikuwa chanzo cha ugomvi huo! Hakukubali tena kutoka na Shabir usiku baada ya kugundua nia yake haikuwa nzuri. Hakutaka kumkorofisha Leah kwa sababu yeye ndiye alikuwa kila kitu kwake.

Matukio hayo yalimfanya Shabir aamue kumpa mke wake likizo kwenda  Bombay,  kupumzika lakini hakuruhusu Victoria aondoke! Leah alilikataa  jambo hilo kwa nguvu zote lakini kwa sababu Shabir alishaamua na tiketi zilishakatwa   ilibidi asafiri ingawa kwa shingo upande, alihisi kitu kingetokea baada ya yeye kuondoka.

“Unalia nini? Si utabaki na bibi Sundra!”Alisema Shabir baada ya ndege kuruka alipomwona Victoria akilia. Bibi Sundra alikuwa bibi kizee mwenye umri wa miaka isiyopungua sitini na tano na raia wa Canada.

Alikuwa mfanyakazi wa ndani ya nyumbani kwa Shabir ni huyo ndiye aliyemfanyia Victoria kila kitu!

“Ninataka kwenda na mama India!”

“Utakwenda safari ijayo kwa sasa baki  nikutafutie shule usome!”

Victoria alilia kutoka uwanja wa ndege hadi  nyumbani kwao ambako bibi Sundra alijaribu kwa nguvu zote kumbembeleza lakini haikuwezekana! Siku hiyo alilala bila kula.

Siku iliyofuata asubuhi Shabir alimwita bibi Sundra kwa maongezi aliyoyaita maalum, bibi alitoka jikoni na kwenda moja kwa moja  hadi sebuleni ambako alimkuta Shabir akimsubiri, asubuhi hiyo Victoria alikuwa bado chumbani amelala!

“I have thought about it twice!”(Nimefikiria mara mbili)

“About what Mr. Shabir?”(Juu ya nini bwana Shabir?)

“It wasn’t right  to let my wife   travell alone to India!”(Haikuwa sahihi kumwacha mke wangu  asafiri peke yake kwenda India) Shabir alisema huku akipigapiga juu ya meza.

“Yes, my son so?”(Ndiyo mwanangu, kwa hiyo) Aliitikia bibi Sundra.

“I have made up my mind and I and Victoria will be travelling to Bombay  this afternoon, so I would like you to take a one month leave till we come back, because we are closing everything!”(Nimebadilisha  maamuzi yangu na mimi na Victoria tutasafiri mchana wa leo kwenda Bombay kwa hiyo naomba uchukue likizo ya mwezi mzima mpaka tutakaporudi, sababu tutafunga kila kitu!) Alisema Shabir kwa msisitizo.

“No problem, when do you want me to start my leave?”(Hakuna tatizo ni lini unataka nianze likizo yangu?)

“Right now! This is you’re cheque!”Sasa hivi na hii hapa ni hundi yako ya malipo)

“Thanks Mr Shabir!”(Ahsante bwana Shabir) Alishukuru bibi Sundra na kuipokea hundi yake lakini moyoni alisikitika kutenganisha na Victoria kwani  alimpenda mno.

Yote hayo yalifanyika Victoria akiwa chumbani akiendelea kulia!Baada ya kukabidhiwa hundi yake alikwenda chumbani na kuanza kupanga nguo   katika sanduku lake kisha  akaenda chumbani kwa Victoria kumwaga!

“Whaaaaaaat”(Nininiiiiii?) Aliuliza Victoria kwa mshangao mkubwa.

“I’m leaving!”(Ninakwenda)

“To?”(Kwenda wapi?)

Bibi Sundra alimweleza Victoria kila kitu walichoongea na Shabir, taarifa hizo zilikuwa  mbaya sana katika moyo wa Victoria alilia  kwa uchungu lakini  hakuubadilisha ukweli.

“No! You cant leave me here, I suspect something bad is gonna happen to me grandma!”(Hapana huwezi kuniacha hapa bibi ninahisi kitu kibaya kitanitokea!)

“No Victoria daddy will take care of you, afterall he  has told me you’re leaving for Bombay this afternoon!”(Hapana Victoria baba yupo atakutunza isitoshe ameniambia mchana huu mnaondoka kwenda Bombay!)

“I don’t think so!”(Sifikirii hivyo)Alisema Victoria  huku akilia mawazo yake hayakuwa sawa, pamoja na upofu wake alihisi kitu kibaya kilikuwa kikija mbele yake!

*******************

Tamaa ya Shabir ilishakithiri, alimtamani Victoria kimapenzi  kupita kiasi na alitaka kutenda naye kitendo kisichostahili lakini uwepo wa mke wake na bibi Sundra ndio kilikuwa kikwazo!

Hapakuwa na safari ya Bombay kama alivyomweleza bibi Sundra bali alitaka abaki nyumbani peke yake na Victoria ili aweze kutimiza haja zake za kimwili kwa mtoto huyo kipofu! Alijua Victoria asingekataa lakini hata kama angekataa alipanga kutumia nguvu na aliamini hakuna mtu angeielewa siri hiyo kwani nyumba yake ilikuwa kubwa   sauti isingesikika nje!

Bibi Sundra aliondoka chumbani na kumwacha Victoria akilia machozi ya uchungu, alitamani kubaki lakini hakuwa na namna yoyote ya kupinga mpango wa mwajiri wake Shabir, alilazimika kuondoka!

“Take care of Victoria Mr Shabir, she is a  nice girl!”(Mtunze vizuri Victoria bwana Shabir ni msichana mzuri sana)

“Yes I will!”(nitafanya hivyo) alijibu Shabir huku akifunga mlango  nyuma ya bibi Sundra. Bibi akawa ameondoka nyumba nzima ikabaki na watu wawili, Victoria na Shabir.

Kwa shabir huo ndio ulikuwa wakati   muafaka wa kutimiza haja zake, lakini aliamua kusubiri hadi usiku uingie ndio afanye mambo yake!mate ya uchu na tamaa yalimdondoka na alitembea hadi chumbani na kumkuta Victoria amelala kitandani akilia machozi. Kwa sababu ya upofu Victoria hakumwona lakini alipomgusa begani Victoria alishtuka.

“Stop crying victoria, I’ m  here  for you!”(Acha kulia Victoria niko kwa ajili yako)

“No daddy! I need Leah, grandmo sundra and Manjit as well!(Hapana baba namhitaji Leah, bibi Sundra na Manjit pia)

“They will be baaack! Dont worry!”(Watarudi tu usiwe na wasi wasi) Shabir aliongea hayo akimpapasa Victory mapaja  na Victoria alihisi kuna tatizo lingetokea.

Shabir alishindwa kufanya jambo lolote baada ya kusikia wafanyakazi wa nje wa nyumba yake wakiongea kwa sauti, aliingiwa na hofu na kushindwa kutekeleza azma yake, aliamua kusubiri usiku uingie! Siku hiyo mishale ya sekunde, dakika na saa kwa Shabir ilitembea taratibu zaidi.

****************

Katikati ya usiku Vicky alikuwa amejilaza kitandani mwake, hakuwa amepata hata lepe la usingizi  noti aliyoachiwa na kaka yake ilikuwa mikononi mwake, alikuwa akimfikiria  Nicholaus! Machozi yalikuwa bado yamkimbubujika  kwa  uchungu  mwili wake ulitetemeka na alihisi jambo lolote baya lilikuwa likija mbele yake ingawa hakujua ni jambo gani.

Ghafla alishutkia kitu kikiifunua neti  ya mbu   iliyokizunguka kitanda chake, alishindwa kuelewa ni kitu gani kilichofanya hivyo! Alinyanyuka kwa haraka na kuketi kitako kitandani huku akitetemeka, muda mfupi baadaye alimsikia mtu akihema.

“Who are yooooou?”(Wewe naniiiiiii?) aliuliza  Victoria lakini hakupata jibu lolote.

“Daddy somebody in  my room!”(Baba kuna mtu chumbani kwangu!) Victoria alimwita Shabir bila kujua ni yeye aliyekuwa ndani ya chumba.

Alimsikia mtu akitambaa  kitandani kuelekea mahali alipokuwa amekaa! Alizidi kuuliza lakini hakujibiwa kitu chochote!

Ghafla alishtukia kitu kizito kikimwanguka kifuani kwake na kumgandamiza kitandani, alijaribu kupiga mayowe lakini alifunikwa na mkono  mdomoni na palepale nguo zake zilianza kushushwa kutoka mwilini mwake, nguo yake ya ndani ilichanwa! Mtu aliyekuwa akifanya yote hayo alikuwa kimya kabisa.

Victoria alijaribu kulia lakini sauti haikutoka  na  kilichofuata hapo kilikuwa ni maumivu ambayo Victoria hakuwahi kukutana nayo maishani mwake! Ilikuwa ni kama kutupwa katika tanuru la moto! Damu nyingi ilikuwa ikimtoka.

“Dadyyyyyyyyyyyyyy!”(Babaaa) alilia Vicky akimwita Shabir hakujua hata kidogo kuwa mtu aliyekuwa amemfanyia unyama ni Shabir..

“Call me Shabir and not your daddy, I love  you  Victoria,  I didnt know  you were a virgin! I’m sorry for what happened!”( Usiniite baba niite Shabir, sikujua wewe ni bikira samahani kwa yaliyotokea) Sauti nzito ya Shabir ilisema na Victoria alishindwa kuamini alifikiri labda ni ndoto..

“Why do you do this to me daddy?”(Kwanini  unanifanyia hivi baba?) Aliuliza Victoria huku  akilia lakini Shabir hakujibu kitu alizidi kumwingilia  bila kujali kiasi cha damu kilichokuwa kikitoka.

Mchezo huo uliendelea mara mbili kwa wiki mpaka mwezi ukatimia, Victoria  hakupenda lakini alifanywa mtumwa wa mapenzi na kuna wakati aliwekewa kisu shingoni kabla ya kuingiliwa! Mwezi mmoja ulipotimia hakuzipata siku zake za hedhi! Ilikuwa si kawaida yake kupitiliza, ilibidi amueleze Shabir na walipokwenda kupimwa mkojo aligundulika  na mimba! Alilia kutwa nzima bila kujua angemwambia  nini Leah akirudi kutoka Bombay, alihisi huo ndio ulikuwa mwisho wa maisha yake! Alitamani kufa kuliko kukutana na Leah ana kwa ana!

 

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Alhamisi hapahapa.

Comments are closed.