TID: Mimi Mnyama Nisameheni

Khalid Mohammed (T.I.D) akipanda jukwaani

Na DENIS MTIMA| GAZETI LA UWAZI| HABARI

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’, aka Mnyama, jana alipata nafasi ya kipekee ya kuzungumza kwenye mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, viongozi wa mkoa waDar es Salaam na waandishi wa habari ambapo kwa mara nyingine alikiri kutumia madawa ya kulevya na kuwaomba radhi watu wote aliowahi kuwakosea kwa sababu ya kutumia madawa.

TID alisema zipo sababu zilizomfanya akatumbukia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ambazo ukifika muda wake atazieleza lakini akatumia nafasi hiyo kuwaomba msamaha watu wote ambao kwa namna moja au nyingine, amewahi kukorofishana nao, au kuwakera kwa sababu hazikuwa akili zake bali ‘influence’ ya madawa.

 

 

Hivi karibuni, TID alikuwa miongoni mwa wasanii kadhaa waliotajwa na Mheshimiwa Makonda kutumia madawa ya kulevya ambapo aliitwa Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa, baadaye akashikiliwa kwa siku mbili na wasanii wenzake kadhaa kabla ya baadaye kuachiwa mahakamani kwa masharti ya kuwataka wakabadili mienendo yao.
“Mimi ni kijana shujaa… mimi Mnyama naomba mnisamehe sana tafadhali,” alisema TID na kushangiliwa.


Loading...

Toa comment