Dimpoz, Diamond Kuachia Ngoma ya Pamoja

Ommy Dimpoz amedokeza ujio wa ngoma mpya ya pamoja na kundi la Blaq Diamond kutoka nchini Afrika Kusini ambao walitamba na smash hit yao ‘’Summer Yo Muthi’’.

 

Blaq Diamond wapo nchini kukamilisha wimbo huo na kwa nyakati tofauti wote kwa pamoja kupitia insta story zao wameonisha shauku ya ujio huo, huku Dimpoz akiandika ‘’Special vist from my boyz Blaq Diamond, i can’t wait for our joint to drop’’.

 

Kundi hilo lilianzishwa mwaka 2010 wakati wamekutana shule na kufanikiwa kuachia album 2 ambazo ni Inqola (2017) na Umuthi (2020) mpaka sasa.


Toa comment