The House of Favourite Newspapers

DINNO KUWAENZI WALIOFARIKI MV NYERERE JUMAMOSI HII

Msanii anayekuja kwa kasi katika gemu la muziki wa kizazi kipya Bongo, Abdallah Manyuti ‘Dinno’ anatarajiwa kuangusha shoo maalum kwa ajili ya kuwaenzi watu wote waliofariki dunia katika ajali ya MV Nyerere, iliyokea Septemba 20, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 230.

Katika event hiyo, Dinno atatambulisha kazi zake mpya aliyoirekodi kwa ajili ya kuwaenzi wote waliopatwa na janga hilo, pamoja na kuzindua kazi zake nyingine mpya zikiwemo nyimbo za Ni Wewe na Nyama.

“Mpango mzima utakuwa ni Jumamosi hii, Oktoba 6, 2018 Mnazi Mmoja kwenye Jengo la Ushirika Ghorofa ya Nne, nawaomba wadau wote wa muziki waniunge mkono,” alisema Dinno ambaye alitambulishwa kwenye gemu na wimbo wake wa Bado Nipo.

Kwa upande wa meneja wa msanii huyo, Mutesigwa Nambiza, amesema mbali na Dinno kutambulisha kazi ya kuwaenzi waathirika wa ajali hiyo, pia siku hiyo watazindua rasmi lebo la Nambiza Entertainment, ambayo kazi yake itakuwa ni kuibua vipaji vipya vya muziki na kuwasimamia wasanii.

Comments are closed.