Kartra

Dismas Ten: Hakuna Kama Haji Manara

OFISA Habari wa zamani wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten, amesema Afisa Habari bora kwenye vilabu vya soka Tanzania ni Hassan Bumbuli wa Yanga na Idrissa Bandari wa Ndanda FC.

 

Ten ambaye pia amewahi kuwa Afisa Habari wa Mbeya City, amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo pia ameweka wazi kuwa kwa upande wa wasemaji hakuna kama Haji Manara wa Simba SC.

 

”Msemaji bora hakuna kama Haji Manara wa Simba SC haswa linapokuja suala la kuzungumza na kuhamasisha,” alisema Ten.


Toa comment