Dk. Mollel: Wanadai Hatutoi Data za Corona ni Ujinga Mtupu – Video

 

SERIKALi imesema matumizi ya data za magonjwa yote, ni kwa ajili ya kuchakata na kisha kuja na mbinu za kisayansi kukabiliana na magonjwa hayo lakini sio swala la kutaka kila wiki Waziri wa Afya aelezale waliofariki na wagonjwa, huko ni kuwatisha wananchi.

 

Hayo yamebainishwa na naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu, Februari 22, 2021.

 

 

“Huu ugonjwa unaoitwa Corona hadi sasa hauna tiba wala njia mahususi ya kuweza kupambana nao, silaha kubwa ya kupambana nao ni kinga ya miili yetu pamoja na kufuata taratibu zinazotolewa na Shirika la Afya duniani (WHO) pamoja na wizara yetu.

 

“Baada ya taharuki ya ugonjwa wa COVID-19 nchini mwaka 2020, Rais wetu Dkt. Magufuli aliweka msimamo, hata wanaopinga msimamo wa sasa wa serikali kuhusu COVID-19, ndio wanafanya yale ambayo Tanzania ilikuwa inaonekana inakosea mwaka 2020 mfano lockdown.

 

“Mwaka jana njia ya Lockdown iliposhauriwa duniani, Rais wetu alisema hatuweki watu lock down, baada ya Tanzania kukataa Lock down mwaka jana, tumejifunza nini? Kati ya wote waliofanya lock down na sisi, nani wameumizwa zaidi na ugonjwa huu wa COVID-19.

 

“Hivi ni nchi gani inaweza kuchukua hatua zaidi na bora za kujikinga zaidi ya Marekani, Uingereza, au nchi zilizoendelea. Leo tunavyozungumza hivi kati ya Marekani na sisi, ni wapi wameumia zaidi na ugonjwa wa COVID-19.

 

 

“Angalieni magonjwa yanayoongoza kwa kuua mwaka 2018, mfano kwa kwa takwimu za kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC), magonjwa ya kushindwa kupumua yalikuwa yanashika namba mbili na hii ni kabla ya ujio wa ugonjwa wa COVID-19.

 

“Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kuanzia mwaka 2006 hadi 2015 kuhusu magonjwa yaliyosababisha vifo zaidi, matokeo yalionesha, Malaria ulikuwa ni ugonjwa unaogoza huku magonjwa ya kushindwa kupumua yakishika nafasi ya pili.

 

 

“Mwaka 2018 kabla ya ugonjwa wa COVID-19 magonjwa yayolikuwa yanaongoza kwa kuua duniani ni magonjwa yaliyotokana na matatizo ya moyo na ugonjwa uliofuatia ni ugonjwa wa kushindwa kupumua. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO).

 

 

“Tunawaambia ndugu zetu wanasheria waliotuletea ushauri wao kuhusu ugonjwa wa COVID-19, tunawaambia kuwa, sheria huamuliwa kwa kufanya midhahalo na kushirikisha wadau, lakini masuala ya afya huamuliwa kwa upembuzi uliofanywa maabara na maamuzi hutokea maabara.

 

 

“Mgonjwa aliyepata Pumu atakwenda hospitalini akiwa hana uwezo wa kupumua, mgonjwa wa kisukari akizidiwa atapelekwa hospitali akiwa hana uwezo wa kupumua, hivyo hivyo mwenye BP na mgonjwa wa COVID-19. Sasa si kila mgonjwa mwenye tatizo la kupumua ana Corona.

 

 

“Tafiti zinasema kwamba, kuna mahusiano ya wasiwasi, msongo wa mawazo(stress), mshituko na kinga ya mwili, ukipata stress kinga ya mwili inashuka, kinga ya mwili ikishuka utapata magonjwa mbalimbali ikiwemo Covid-19.

 

 

“Wanasema Tanzania haitoi data, matumizi ya data za magonjwa yote, ni kwa ajili ya kuchakata na kisha kuja na mbinu za kisayansi kukabiliana na magonjwa hayo lakini sio swala la kutaka kila siku Waziri wa Afya aelezale kwenye TV waliofariki, wagonjwa, waliozikwa ni ujinga mtupu, unatishia taifa na kufanya lisitulie,” amesema Dk. Mollel.

 

Toa comment